Movers & Shekers wajadili ukuaji muziki kwenye Sauti za Busara 2018

0
269

Wasanii na Wadau wa Muziki wamekutana kwa pamoja kwenye kongamano la jukwaa la Movers & Shekers kujadili juu ya ukuaji wa muziki Barani Afrika katika tamasha la 15 la Muziki la Kimataifa la Sauti za Busara 2018.

Kongamano hilo la Movers & Shekers lenye lengo la kukuza mafunzo ya Sanaa na muziki limekuwa chachu kwa Wasanii shiriki kujifunza mambo mbalimbali pamoja na kubadilishana uzoefu na Wasanii pamoja na wadau wa Muziki.

Aidha, leo mapema washiriki kama Isack Abeneko kutoka Tanzania, Siti Amina kutoka Zanzibar, Mzungu Kichaa (Tanzania-Denmark) na Kabubi Herman kutoka kundi la Bayimba (Uganda) waliweza kuungana na wadau hao katika kushiriki kongamano hilo.

Wasanii hao, wameweza kuujadili muziki wa Afrika na namna wanavyoweza kuendelea kuukuza zaidi ili kuleta mafanikio kwa njia moja ama nyingine.

Hata hivyo, Wadau wa muziki wameweza kutoa mawazo yao namna ya kuwasaidia wasanii wa Afrika hasa kwa kuinua muziki wao wennye lengo la kuleta mageuzi chanya ya kimuziki Afrika.

NA ANDREW CHALE-BONGONEWS,ZANZIBAR

Mwanamuziki Kabubi Herman wa kundi la BAYIMBA la nchini Uganda akizungumzia aina ya Muziki wanaoimba pamoja na njia ya Wasanii wa Afrika kuweza kufuata misingi ya muziki wa Kiafrika. Kulia kwake ni  Msanii Isack Abeneko kutoka Tanzania,  na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Busara Promotions waandaaji wa tamasha hilo la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud.

Wadau wa Muziki wakifuatilia kongamano hilo mapema leo Februari 9,2018

Crew ya Sauti za Busara wakiwa mitamboni kwenye Kongamano hilo leo

Mwanamuziki Mkongwe na Mshehereshaji wa Muziki nchini, Carola Daniel Amri Kinasha akichangia mada juu ya ukuaji wa muziki Barani Afrika kwenye kongamano hilo leo

Yusuf Mahmoud akiendesha jukwaa hilo

Mdau wa Muziki Jens Cording kutoka Musicinafrica.net akichangia mada namna ya kuinua muziki wa Afrika katika kongamano hilo mapema leo

Mdau wa Muziki Jens Cording kutoka Musicinafrica.net akichangia mada namna ya kuinua muziki wa Afrika katika kongamano hilo mapema leo

Abdi Rashid Jabru kutoka ROOTS INTERNATIONAL  akichangia mada kwenye kongamano hilo mapema leo

Mwanamuziki Siti Amina kutoka Visiwani Zanzibar akielezea namna ya uzoefu wake katika muziki ikiwemo ushiriki wake wa tamsha la Sauti za Busara 2018

Mtalaam na mtafiti katika muziki kutoka Marekan, William Bissell akichangia mawazo namna ya muziki wa Afrika uweze kukua zaidi mapema leo kwenye kongamano hilo

Mtalaam na mtafiti katika muziki kutoka Marekan, William Bissell akichangia mawazo namna ya muziki wa Afrika uweze kukua zaidi mapema leo kwenye kongamano hilo

Abdi Rashid Jabru kutoka ROOTS INTERNATIONAL  akichangia mada kwenye kongamano hilo mapema leo

Mdau wa Muziki kutoka mtandao wa kuuza muziki kwa wasanii wa Mkito, Ismail Lossini akichangia tukio hilo

Mdau wa Muziki kutoka mtandao wa kuuza muziki kwa wasanii wa Mkito, Ismail Lossini akichangia tukio hilo

Mdau wa muziki Afrika Julie Olum wa mtandao wa FRAMEAMBIATION.COM wa Nchini Kenya akichangia mada namna ya wanamuziki kutumia platifomu ya mtandao ili kukuza na kujitangaza zaidi

Yusuf Mahmoud akipeana mikono na muziki Abeneko wakati wa tamasha hilo

Msanii Siti Amina akijadiliana jambo na Mdau  wa muziki wakati wa kongamano hilo

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here