Sikinde wakonga nyoyo tamasha la Sauti za Busara,Zanzibar

0
156

Bendi kongwe ya muziki wa dansi nchini, Mlimani Park ‘Sikinde’ usiku wa jana Februari 8,2018 wamekonga nyoyo za umati mkubwa wa watu wa Mataifa mbalimbali walio furika kwenye onesho kubwa la Kimataifa la Muziki la Sauti za Busara, ambalo kwa mwaka huu linafanyika kwa siku nne, Februari 8-11, Visiwani hapa.

Sikinde ambao walipanda jukwaani majira ya saa Tatu usiku na kulishambulia jukwaa kwa nyimbo zao mbalimbali zikiwemo za zamani na za sasa, Viunga vya Ngome Kongwe vililipuka kwa shangwe kwa nyimbo zao hizo.

Miongoni mwa nyimbo hizo ni pamoja na Majaliwa yake Mungu kuuona mwaka, Gama, Furahi na Mwanasikinde na Isaya.

Wakizungumza na mtandao huu baada ya onesho lao hilo visiwani hapa, bendi hiyo ambayo kwa mwaka huu wamefikisha miaka 40, tokea kuanzishwa kwao hapa nchini, wafurahia na kupongeza kuchaguliwa kwao katika tamasha hasa kuonesha muziki wao wa dansi katika jukwaa kama  hilo la Kimataifa.

Sikinde kwa mwaka huu ni wa nne kushiriki tamasha hilo huku wakieleza kuwa, limekuwa likibadirika kila mwaka na kuwapongeza waandaaji wa wake kwani wamesaidia kuupaisha muziki wa Tanzania, na Afrika kwa ujumla.

Akielezea kwa kina, Mwanamuziki Mkongwe wa bendi hiyo ambaye pia ni Mtafiti wa muziki na muimbaji, Mzee Hasan Bitchuka ambaye ni miongoni mwa wachache waliobakia katika bendi hiyo, amefafanuwa kuwa, kila wanaposhiriki tamsha hilo kubwa nchini na Afrika kwa ujumla wamekuwa wakishuhudia mabadiliko makubwa kwenye muziki.

“Mwaka huu tamsha limebadilika sana. tunashukuru watu kuupokea muziki wetu.. tunaomba uongozi wa Busara utuite tena kwenye kushiriki pia tungefurahia kama tungekuwapo wakati wa kufunga tamasha kwani mashabiki wetu bado wanatamani kutuona tena tukiimba jukwaani” alisema Bitchuka.

“Ili tamasha la Sauti za Busara tunalipenda sana. Limekuwa chachu ya maendeleo kwa vikundi na wanamuziki kuonekana Ulimwenguni. Alieleza Bitchuka.

Kwa upande wake, Mwanamuziki mwingine wa bendi hiyo, Abdalla Temba ambaye kwa sasa amekuwa chagua kubwa ya bendi hiyo kwa kuweza kuimba nyimbo za wanamuziki wa zamani akiwemo marehemu Mzee Gurumo ambapo amekuwa akiimba jukwaani sawa sawa na alivyokuwa Mzee Gurumo hii ni pamoja na kuiga Sauti.

“Kuna nyimbo zetu zipo studio kwa sasa ambazo ni mpya. wakati wowote tutazitoa hewani kwa mashabiki wetu. Tunawaomba wakae mkao wa kutupokea.

NA ANDREW CHALE-BONGONEWS,ZANZIBAR

Wanamuziki wa Bendi ya SIKINDE wakiwa jukwaani usiku wa jana Februari 8,2018 wakati wa onesho la kwanza katika ufunguzi.

Mwanamuziki Abdalla Temba ambaye amerithi mikoba ya Marehemu Mzee Gurumo akilishambulia jukwaa hilo la Sauti za Busara jana Februari 8,2018 wakati wa onesho la kwanza katika ufunguzi.

Wanamuziki wa Bendi ya SIKINDE wakiwa jukwaani usiku wa jana Februari 8,2018 wakati wa onesho la kwanza katika ufunguzi.

Photo credit: Rashde Fidigo- Busara

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here