Rais Magufuli ampandisha cheo na kumteua Kamishna wa Polisi Zanzibar

0
215

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Februari, 2018 amempandisha cheo na kumteua Bw. Mohamed Hassan Haji kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imefafanua kuwa
Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo Bw. Mohamed Hassan Haji kutoka
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna wa Polisi (CP), na kisha
kumteua kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.

Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji amepandishwa cheo na kuteuliwa
kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar kuanzia leo tarehe 10 Februari, 2018.
Kabla ya uteuzi huu Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji alikuwa Mhasibu
Mkuu wa Polisi Zanzibar.

Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji anachukua nafasi iliyoachwa wazi na
Kamishna wa Polisi Hamad Omar Makame ambaye amestaafu.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Februari, 2018

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here