Saida Kaloli arejea enzi ya Muziki wake,akonga nyoyo Sauti za Busara 2018

0
690

Mwanamuziki Saida Karoli anayeimba nyimbo za asili ya kabila la Kihaya nchini kwa sasa ameweka wazi kuwa amerejea rasmi katika enzi zake katika tasnia ya muziki hapa nchini huku akitamba kufanya muziki mpaka anakufa.

Akizungmza katika mahojiano maalum na mtandao huu wa BONGONEWS.CO.TZ Mjini hapa, Saida Kaloli amesema kuwa mashabiki wake wakae mkao wa kura kwani amejipanga na atafanya muziki mpaka kifo kitakapomuita.

“Kwa sasa ndio nimerejea rasmi katika muziki. Mimi sina muda wa mwaka gani nitaacha bali nitaendelea na muziki mpaka kufa kwangu” alieleza Saida Kaloli.

Aidha, amefunguka kuwa, kutokana na muziki kuwa katika damu yake, mwae pia amefuata nyao zake lakini katika Muziki wa Bongo Fleva.

“Mimi muziki upo katika damu. Mwanangu wa kiume nae anafanya muziki lakini sio kama huu wangu wa asili, Yeye anafanya muziki wa Bongo fleva na hii ni kutokana na kukulia maisha ya mjini” alifunguka Saida Kaloli.

Mwanamuziki huyo ameweka wazi kuwa, kwa sasa kurejea kwake katika muziki hana Meneja bali ana watu wenye mapenzi mema na kazi zake akiwa anasaidiana nao katika kusukuma gurudumu la muziki wake huo.

Saida Kaloli akielezea tamasha la Sauti za Busara 2018, amesema limemfanya ajione wa tofauti na kupongeza mashabiki wa Sauti za Busara kwa kumpigia shangwe katika onesho lake zima jukwaani.

Saida Kaloli amepanda jukwaani majira ya saa tano kamili usiku na kupagawisha kwa nyimbo zake mbalimbali zikiwemo zile za zamani na za sasa huku muda wote akipata shangwe kutoka kwa mashabiki wa tamasha hilo waliofurika katika jukwaa hilo la ndani ya Ngome Kongwe.

NA ANDREW CHALE-BONGONEWS,ZANZIBAR

Saida Kaloli akiimba jukwaani 

Umati uliofurika

PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE-BONGONEWS,ZANZIBAR

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here