Tamasha la Sauti za Busara kuwa endelevu, Wadau waombwa kulidhamini

0
160

Tamasha la Muziki la Kimataifa la Sauti za Busara linaloendelea visiwani hapa limedizi kupamba moto huku mashabiki na wapenda burudani ya muziki wakikonga nyoyo zao kwa muziki safi na wenye kuvutia katika viunga vya Mji Mkongwe ndani ya Ngome Kongwe.

Usiku wa jana Februari 9,2018, Mwenyekiti wa Bodi ya Sauti za Busara, Mh. Simai Mohammed amesema anataka kuona tamasha linakuwa endelevu na mafanikio huku akiwaomba wadau na wafanyabiashara wote wakiwemo wa Visiwani humo na Tanzania Bara kujitokeza kutumia fursa hiyo ya kulichangia tamasha.

“Kwa niaba ya Bodi, na niombe kutumia fursa hii kwa wafanyabishara na wadau wote watumie fursa ya uwepo Sauti za Busara ili waweze kujiimalisha kwani tamasha ili kwa sasa si la Wazanzibari bali ni letu sote” alieleza Simai.

Pia amesema kuwa, wafanyabiashara kutoka Mbeya ama Arusha ama kwingine wanaweza kujitokeza kuungana nao na kusaidia kutokana na mambo mbalimbali ya kiuchumi na kuongeza kuwa, kila mmoja anayo nafasi ya kujitokeza kulichangia tamasha ili liendelee kuwa chachu kwa ukuaji wa Utalii, Uchumi na Utamaduni kwa ujumla.

Aidha, Mhueshimiwa Simai Mohammed ameweza kuitambulisha Bodi pamoja na uongozi mzima wa Busara Promotions kwa namna walivyoweza kujiandaa mpaka kukamilisha tamasha hilo msimu huu ambalo linakuwa la 15 tokea kuanzishwa kwake.

Tamasha la Sauti za Busara kwa mwaka huu limebeba kauli mbiu ya “Kuunganishwa na Muziki”, Waafrika na wageni kutoka katika kila pembe ya dunia, linajumuisha vikundi zaidi ya 40, ambavyo vinaendelea kutoa burudani kuanzia hiyo Februari 8,2018 na kutarajia kufikia tamati hiyo kesho Februari 11,2018.

Miongoni mwa wasanii ambao washiriki kwa mwaka huu ni pamoja na Mwanamuziki wa nyimbo za Asili la kabila la Kihaya, Saida Kaloli na wanamuziki wengine wengi wakiwemo Zakes Bantwini (Afrika Kusini), Kasai Allstars (DRC), Somi (Uganda/USA), Ribab Fusion (Morocco), Kidum na tha boda boda band (Burundi/Kenya), Mlimani Park Orchestra (Tanzani), Grace Matata (Tanzania) na Msafiri Zawose (Tanzania).

NA ANDREW CHALE-BONGONEWS,ZANZIBAR

Wajumbe wa Bodi na watendaji wa Busara Promotions wakiwa wameshikana mikono kwa pamoja jukwaani wakati wa utambulisho huo

Wajumbe wa Bodi na watendaji wa Busara Promotions wakiwa kwa pamoja jukwaani wakati wa utambulisho huo

Mwenyekiti wa Bodi ya Sauti za Busara, Mh. Simai Mohammed akihamasisha Umati wa mashabiki wa muziki wa tamsha la Sauti za Busara waliojitokeza kwenye tukio hilo usiku wa jana Februari 9,2018. 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Photos credit by Sauti za Busara Photographers team

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here