Mapanya Band waonesha uwezo wao Sauti za Busara 2018

0
411

Bendi ya muziki inayowajumuisha vijana Saba (7) wanaosoma chuo cha Muziki Dhow Countries Music Academy (DCMA) wajulikanao kama Mapanya Band, usiku wa leo Februari 11,2018 wameonesha uwezo wao kwenye tamasha la 15 la Kimataifa la Muziki Sauti za Busara.

katika shoo hiyo waliopanda majira ya saa mbili usiku, vijana hao licha ya kuwa na umri mdogo, wameweza kukonga nyoyo za mashabiki waliofurika kushuhudia Sauti za Busara mwaka huu tamasha ambalo linfikia tamati hii leo.Hata hivyo, vijana hao wameeleza kuwa, kwa sasa wana nyimbo tatu ambazo tayari wamesha rekodi huku zingine zikiwa mbioni endapo watapata wadhamini.

Akizungumza na mtandao hu, mmoja wa viongozi wa kundi hilo, Frednand Ngomoi amesema wameamua kujiita Mapanya, hii ni kutokana na kuwakilisha sauti ya jamii ya chini dhidi ya sauti kubwa za mapaka ambao ni jamii iliyojuu.

“Nyimbo na aina ya muziki wetu ni wa kikwetu tu. Sie tunawakilisha sauti ya jamii iliyochini kwa sauti yao ni panya na walio juu sauti yao wao ni paka, hii ni taswira tu ambayo kitu kinaweza kujengwa kwa fikra.” alieleza Ngomoi.

Kwa sasa kundi hilo wapo chini ya Saraha Hausheer raia wa Swis ambaye ni kama mlezi wao kwa sasa ambaye wanasema kuwa, wanaamini watafika mbali katika tasnia ya muziki.

Mapanya Band kundi lililoanzishwa miaka miwili iliyopita huku wakiwa bado ni wanafunzi wa chuo hicho cha muziki ambapo wameweka wazi kuwa safari yao ya muziki ndio imeanza na Sauti za Busara 2018, ndio mara ya kwanza wanashiriki hivyo kwao ni kama milango imefunguka, wamebainisha Mapanya.

NA ANDREW CHALE-BONGONEWS,ZANZIBAR

Kundi la Mapanya wakifanya mkutano na mtandao huu

Kundi la Mapanya wakiwajibika jukwaani Sauti za Busara 2018, usiku wa leo Februari 11,2018.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here