Msafiri Zawose aendeleza ujuzi wa ngoma za kabila la Wagogo Sauti za Busara 2018

0
184

Msanii wa nyimbo za Asili la kabila la Wagogo, Msafiri Nzawose kutoka (Dodoma na Bagamoyo) usiku wa Februari 11,2018 ameweza kukonga nyoyo za mashabiki waliofurika kwenye kilele cha tamasha la Kimataifa la Muziki la Sauti za Busara ambalo limefikia tamati usiku huu.

katika onesho hilo, Msafiri ambaye alipanda na bendi yake waliweza kuonesha ujuzi wa kupiga ala za muziki la kabila hilo la Wagogo kwa ustadi mkubwa.

Miongoni mwa nyimbo alizopiga jukwaani usiku huu ni pamoja na Mishemishe, Hapa Duniani,Miamwana, Makanyegale, Inyima na nyingine ambazo zipo mpya.

Aidha, Mzawose amesema kuwa, Mwaka huu Septemba anatarajia kuachia albam yake mpya inayokwenda kwa jina la Uhamiaji ambayo anabainisha kuwa atazunguka sehemu mbalimbali kusambaza muziki huo ikiwemo kwenye majukwaa makubwa.

Akielezea tamasha la Sauti za Busara 2018, amesema kuwa, tamasha linabadirika kila mwaka na waandaaji wanajitahidi.

“Naona kila mwaka tamasha linabadirika sana. Mabadiliko haya ndio ambayo yanatufanya na sie wasanii tuwe tunajipanga vyema ili tuweze kufikia ukubwa wenyewe wa tamasha.” alieleza Msafiri Zawose.

Katika ushiriki wake kwenye Sauti za Busara, Msafiri anasema ameweza kushiriki mara nyingi kwa kufika kwenye tamasha hilo kwa bendi tofautitofauti.

NA ANDREW CHALE-BONGONEWS,ZANZIBAR

Wasanii wa kundi la Msafiri Zawose wakiwa jukwaani wakati wa tukio hilo

Wasanii wa kundi la Msafiri Zawose wakiwa jukwaani wakati wa tukio hilo

Msafiri Zawose akiwa jukwaani Sauti za Busara 2018

Msafiri Zawose akiwa jukwaani Sauti za Busara 2018

PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE-BONGONEWS,ZANZIBAR

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here