Rais Magufuli amteua Meja Jenerali Yakubu kuwa Mnadhimu Mkuu JWTZ

0
92

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 14 Februari, 2018 amemteua Meja Jenerali Yakubu Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Pamoja na uteuzi huo, Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo kutoka Meja
Jenerali na kuwa Luteni Jenerali.

Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed anachukua nafasi ya Luteni Jenerali
James Alois Mwakibolwa ambaye amestaafu.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapandisha vyeo kutoka Brigedia Jenerali na
kuwa Meja Jenerali wafuatao;

1. Brig Jen. J.G. Kingu
2. Brig Jen. M.S. Busungu
3. Brig Jen. R.R. Mrangira
4. Brig Jen. B.K. Masanja
5. Brig Jen. G.T. Msongole
6. Brig Jen. A.F. Kapinga
7. Brig Jen. K.P. Njelekela
8. Brig Jen. A.S. Bahati
9. Brig Jen. M.E. Mkingule
10. Brig Jen. S.S. Makona

Mabrigedia Jenerali wote waliopandishwa vyeo watapangiwa vituo vya kazi
baadaye.

Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed
ataapishwa kesho tarehe 15 Februari, 2018 saa 5:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es
Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

14 Februari, 2018

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here