Makamu wa Rais Samia aanza ziara ya siku tano Mkoani Simiyu

0
603

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa mkoa wa Simiyu kuhakikisha kila shule ya sekondari inayojengwa inajengwa ikiwa na maabara.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi
Lamadi wilaya ya Busega mkoani Simiyu ikiwa siku yake ya kwanza ya
ziara ya siku tano mkoani humo.

Makamu wa Rais ambaye alianza ziara yake kwa kuweka jiwe la
msingi la ujenzi wa mradi wa maji uliopo Kiloleli ambapo mradi huo
ukikamilika utasaidia kupatikana kwa maji safi na salama kwa vijiji
vitatu na utagharimu shilingi za kitanzania bilioni 1.6 ambapo ujenzi
wake umefikia asilimia 80%.

Makamu wa Rais aliwapongeza wananchi kwa kuunga mkono juhudi
za Serikali ya awamu ya tano katika uwekezaji na uendelezaji wa viwa
nda ambapo mpaka sasa kuna viwanda 14 vya usindikaji wa pamba
na viwanda vidogo vidogo vya usindikaji mazao 1,035.

“Nawapongeza kwa mkakati wa kuzalisha bidhaa za afya zinazotokana na pamba na maji ya drip”

Makamu wa Rais aliwaambia wananchi hao kuwa hadi mwisho wa mwezi huu chupa milioni 2 za dawa za kuuwa wadudu wanaoshambulia pamba zitakuwa zimesambazwa.

Mwisho Makamu wa Rais aliwataka Viongozi na Watendaji kushirikiana na wananchi kwani ushirikiano Katiak Ziara hiyo Makamu wa Rais aliweka pia jiwe la msingi la ujenzi
wa Nyumba za Viongozi wa Serikali zilizopo Nyaumata.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wakazi wa Mji wa Bariadi mara baada ya hafla fupi ya Barabara kupewa jina la Samia Suluhu Avenue. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka pamoja na Watoto wa Mji wa Bariadi mara baada ya hafla fupi ya Barabara kupewa jina la Samia Suluhu Avenue. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here