MANET wawasilisha mapendekezo ya sera na sheria usimamizi Mazingira nchini

0
117

Serikali nchini imetakiwa kukazia pamoja na kusisitiza agizo la ulazima kwa taasisi zote za umma na binafsi kutumia majiko sanifu na njia nyingine za kupata nishati ya kupikia kulingana na mazingira ya taasisi ili kutunza misitu ya asili na malisho ya wanyama.

Hayo yalibainishwa na   Asasi za Mazingira nchini wakati wakiwasilisha  mapendekezo yao  kuboresha Sera na Sheria zinazosimamia mazingira na maliasili nchini  katika mkutano wao na Wabunge marafiki wa mazingira Mkoani Dodoma hivi karibuni.

Mapendekezo hayo yaliyowasilishwa na Makamu mwenyekiti wa bodi ya mtandao wa asasi za mazingira nchini (Mazingira Network – MANET) Bi. Secelela Balisidya yamependekeza kuwepo kwa haja kwa serikali kusimamia ukamilikaji wa baadhi ya kanuni za Usimamizi na utekelezaji  wa sera na sheria za mazingira na maliasili ambazo hazipo.

Serikali kuangalia zaidi Kanuni za kusimamia Nishati Jadidifu na Tungamo-Taka (Mfano kutokamilika kwa Biomass Strategy of Tanzania (BEST) na Kanuni zinazopaswa kuzisaidia sheria ziweze kutekelezeka ni moja ya mapendekezo yaliyotolewa.

“Usimamizi usioridhisha wa sheria unatoa mwanya wa kuendelea kwa uharibifu wa mazingira nchini (kwa mfano migogoro itokanayo na matumizi ya maji na malisho kati ya wafugaji na wakulima, wanyamapori na wananchi wanaozunguka hifadhi, pia matumizi yasiyo endelevu ya Tungamo-Taka (Biomass)  hasa kuni na mkaa”taarfia hiyo ilieleza.

Akifungua semina hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya MANET Bw. Zuberi Mwachulla alisema ni muhimu watunga sera na asasi za kiraia kuwa na ushirikiaon ili kuleta maendeleo ya wananc kwa kuwa wote wanafanya kazi zinazolenga kumletea maendeleo mwanachi nchini Tanzania.

Naye Mwenyekiti wa chama hicho cha TAPAFE Mh. Jeetu Patel amesema ni muhimu mikutano kama hiyo kufanyika mara kwa mara ili kuwapa nafasi wabunge kupata taarifa zinafanyiwa utafiti na asasi za kiraia kwa ajili ya kuboresha majadiiano Bungeni na kuleta maendeleo kwa wananchi. 

Semina hiyo iliwezeshwa na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira Duniani  (WWF) – Ofisi ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) ilikutanisha mitandao minne inayojihusisha na utunzaji na usimamizi wa mazingira ya MANET, Sustainable Energy Forum (SEF), Northern Coalition (NC) na Mtwara Regional NGOs Network (MRENGO) 

Bi Secelela Balisidya Makamu mwenyekiti wa bodi ya Mtandao wa Asasi za Mazingira nchini MANET

Mwenyekiti wa TAPAFE Mh Jeetu Patel akifungua semina ya wabunge na Asasi za kiraia za Mazingira Mjini Dodoma.

Picha ya pamoja

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here