Serikali yaanza mazungumzo na BHARTI AIRTEL inayomiliki AIRTEL Tanzania

0
139

Mazungumzo kati ya Kamati Maalum iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Kampuni ya Bharti Airtel inayomiliki hisa katika kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania yameanza rasmi leo tarehe 12 Machi, 2018 Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo kamati iliyoundwa na Mhe. Rais Magufuli inaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi na timu ya Bharti Airtel inaongozwa na Mwanasheria Mkuu wake Bw. Mukesh Bhavnani.

Mazungumzo hayo yanalengo la kufikia makubaliano yatakayokuwa na tija
kwa pande zote mbili (Serikali ya Tanzania na Bharti Airtel) na kuimarisha
sekta ya mawasiliano nchini Tanzania.

Kampuni ya Bharti Airtel iliomba kufanyika kwa mazaungumzo hayo baada ya kamati iliyofanya uchunguzi kuhusu umiliki wa kampuni ya Airtel Tanzania kuwasilisha ripoti yake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
12 Machi, 2018

Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akiongoza ujumbe wa serikali katika mazungumzo na mwanasheria mkuu wa kampuni ya Bharti  Bw. Mukesh Bhavnani  pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa  kampuni hiyo Bi. Tina Uneken-van de Vreede na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano  walipoanza rasmi mazungumzo yenye lengo la kufikia makubaliano yatayokuwa na tija kwa pande zote mbili kuhusu umiliki wa Airtel Tanzania leo Machi 12, 2018 jijini Dar es salaam.

Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akipeana mikono na mwanasheria mkuu wa kampuni ya Bharti  Bw. Mukesh Bhavnani walipokutana  kwa ajili ya kuanza rasmi kwa mazungumzo kati ya Serikali na kampuni hiyo kwa lengo la kufikia makubaliano yatayokuwa na tija kwa pande zote mbili kuhusu umiliki wa Airtel Tanzania leo Machi 12, 2018 jijini Dar es salaam

PICHA ZOTE NA IKULU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here