Mwakyembe apongeza Mikoa 18 na Halmashauri 9 zinavyoendesha tovuti zao

0
190

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amezipongeza Sekretariet za Mikoa 18 pamoja na Halmashauri 9 zinazofanya vizur katika Uhuishaji wa Taarifa kwenye Tovuti zao.

Mhe. Mwakyembe ameyasema hayo kwenye Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini unaofanyka katika Ukumbi wa Aicc, Jijini Arusha.

Mhe. Mwakyembe amesema Kupitia Ofisi ya Rais-Tamisemi tulilenga kuboresha Utoaji wa Taarifa kwa Umma na katika kufanikisha hilo March,2017 tulizindua Tovuti za Mikoa pamoja na Halmashauri ili kuongeza uwazi na uwajibikaji wa Serikali kwa wananchi wake.

“ Katika Ufunguzi huo tulisisitiza Tovuti hizo ziwe Majokofu ya habari na Sio Magofu lakini katika maeneo mengine hawawajibiki ipasavyo kuweka taarifa mbalimbali za maendeleo katika Tovuti hizo” Alisema Mwakyembe

Aliongeza kuwa Halmashuri zinazofanya vizuri ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mufindi, Kibaha, Mlele,Kinondoni, Ilala pamoja na Ubungo.

Kwa Upande wa Sekretariet za Mikoa zilizofanya Vizuri ni Mwanza, Mara, Kagera, Tabora, Shinyanga, Simiyu, Arusha, Tanga, Lindi, Mtwara,Ruvuma, Rukwa, Mbeya, Iringa, Morogoro, Geita, Katavi na Songwe.

Mkutano huu wa Mwaka ambao hufanyika kila mwaka umehusisha Maafisa Mawasiliano wa Serikali zaidi ya Mia Tatu kutoka katika Wizara, Taasisi, Idara za Serikali, Sekretariet za Mikoa pamoja na Halmashauro na utafanyika kwa muda wa Siku Tano.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here