Makeke aja na mtindo wa ubunifu wa vazi la Ungo ‘LUPAHERO’

0
308

Baada ya uzoefu mkubwa katika matumizi ya mapishijikoni, ungo umejizolea umaarufu mkubwa baada ya kuingizwa rasmi katika tasnia ya sanaa hususani katika ubunifu wa mavazi na kupewa jina la LUPAHERO na Jocktan Makeke.

Maanaya LUPAHERO

Ubunifu huu wa mavazi umepewa jina la LUPAHERO ambalo ni mchanganyiko wa majina mawili ambayo ni  LUPAPIKE, neno la kinyakyusa lenyemaana ya ungo na neno la pili ni LUHELO, ambalo ni neno la kihehe lenye maana ya ungo.

Muunganiko wa maneno haya mawili umelenga kuleta dhana ya ushujaa kutokana na ladha ya mavazi hayo kuwa na dhima hiyo, huku neno Luhelo likitamkwa herufi za mwisho kama Hero, herufi  L ikibadilishwa kuwa  R  ilikupata neno hero la kingereza lenye maana ya shujaa na kukamilisha maana halisi ya ubunifu huo kuwa shujaa wa ungo.

Jinsi wazo lilivyopatikana

Katika maandalizi ya onyesho la  kwanza kufanywa chini ya MAKEKE INTERNATIONAL  lililofahamika kama I AM MAKEKE  ndipo wazo hili la lupahero lilipozaliwa. Kwa mujibu wa MAKEKE INTERNATIONAL ili mchukua muda mrefu kupata wazo la kufanya katika onyesho hilo licha ya kua na bidhaa nyingi za kubuni nguo mbalimbali ofisini kwake.

Baada ya kuwaza kwa muda mrefu ndani ya ofisi alitoka nje na kurudi baada ya kutuliza akili lakini wakati akirudi aliuona ungo kupitia dirisha uliokua umetundikwa ukutani kama pambo la ofisi ambapo aliamua kuuchukua na kukaa nao huku kichwa kikiendelea kuwaza na kuwazua niwazo gani ataonyesha kwenye onyesho lililokua mbele yake.

Baada ya kuwaza kwa masaa kadhaa wazo lilimjia na kutaka kutoboa ungo aliokua nao kwa kiasi cha kuweza kuvaa shingoni ambapo alifanya hivyo na kupata ladha ya mapambo ya shingoni ya kimasai ila katika mwonekano wa ungo na ndipo alipoanza kufikiria mikato mingine ambayo ungo unaweza kuingia na kudhihirisha ubunifu wa ungo kama vazi.

Baada ya kupata yote hayo makeke alichukua daftari na kuanza kuchora kila alichokua amekiwaza kwa ufanisi zaidi na kufanyia kazi kwa muda aliokua nao hali iliyofanya ubunifu wa ungo kutumika kwa mara ya  kwanza  katika tamasha la I AM MAKEKE mpaka hivi sasa.

Mikato yaLupahero

Hapa zitakaa picha za mikato ya ungo kama ya shingoni, mikono ni mgongoni kifuani na kadhalika

MAKEKE INTERNATIONAL imelenga zaidi kujenga dhana  ya ushujaa na asili ya kiafrika ili kujenga mazingira ya kuweza kujiamini na kujua  kuwa wewe ni bora zaidi kutokana na jinsi ulivyo kama mwafrika na shujaa  kwa kila jambo.

Follow us o Facebook  @makeke international Instagram @makeke international  blog makekeinternational.blogspot.com

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here