Jinsi ya kuuandaa muhogo wa nazi na samaki

0
130

MUHOGO WA NAZI
Mahitaji
Samaki 1 mkate vipande
Muhogo 1 mkubwa au 2 ya kiasi (nimetumia wa pakti )
Nazi/tui zito vikombe 3
Kitunguu saum punje 2
Pilipili boga/hoho jekundu na kijani
Chumvi kiasi
.
.. menya ukate kate na ukoshe muhogo, uuteleke na maji vikombe 2 , uchemshe ulainike kiasi tu usiwe mlaini sana (si lazima kama sio mgumu) – kama ni mchungu umwage maji
.
.pembeni chemsha Samaki, Kitunguu saum na chumvi mtie maji kiasi na akishawiva abakie na supu kiasi ya kikombe 1

.. muhogo ukishakulainika, maji yamekauka au umeshayamwaga, tia supu (pekee) ya samaki, pilipili boga iliyokatwa katwa, na nazi/tui, onja chumvi ikihitajika engeza. Funika kwa moto wa kiasi mpaka ubakie na rojo size unayopenda, epua weka samaki juu, wacha upoe kiasi na ENJOY. Ni mtaam saana. #shunaskitchen Kwa recipe zaidi gusa haya maandishi ya blue https://www.youtube.com/channel/UCaXaogqm-ndd4ofuxERc_kg . Asanteni

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here