KWESE Free Sports Tanzania (TV1) waungana na TBC kuonesha Kombe la Dunia

0
449

KWESE Free Sports Tanzania (KFS) imetangaza rasmi leo kuwa ni kituo pekee nchini kitakachorusha matangazo ya michuano ya Kombe la Dunia (FIFA World Cup 2018) bure inayotarajiwa kuanza tarehe 14 Juni 2018 mpaka kumalizika kwake tarehe 15 July 2018 nchini Urusi kupitia chaneli ya TBC.

KFS Tanzania wakishirikiana na kituo cha televisheni cha taifa, TBC, watarusha matangazo hayo moja kwa moja (LIVE) kwa michezo yote zaidi ya 60.

Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa tukio la kusainiana mikataba Mkurugenzi wa KFS Tanzania, Joseph Sayi  na Shirika la Utangazaji la Taifa la TBC, Mkurugenzi huyo amesema kuwa: “Michezo ni moja kati ya maeneo muhimu katika tasnia ya burudani nchini Tanzania na duniani kote. Ni kwa sababu hii, KFS Tanzania, inajivunia kuwapatia fursa watazamaji wake ya kutazama moja kwa moja ya mashindano makubwa ya kimichezo duniani.

Kudhihirisha lengo letu la kutoa kipaumbele katika michezo na burudani kwa watazamaji wetu, tunawaleletea michezo ya Kombe la Dunia (FIFA World Cup 2018) moja kwa moja mpaka majumbani mwao bila gharama yoyote. FIFA World Cup ni michuano inayotazamwa na watu wengi kuliko yote duniani ikiwa na washabiki wapatao bilioni 3, inayotoa fursa maalumu inayokuja mara moja tu kila baada ya miaka minne kwa biashara mbali mbali kutangaza bidhaa zao.” alieleza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayoub Rioba  amesema kuwa wamejipanga kuonesha kombe hilo kwa kiwango cha hali ya juu na watazamaji watafurahia michuano hiyo kutoka Nchini Urusi huku pia ikirushwa kwa lugha ya Kiswahili.

“Tunafuraha kubwa kufikia hatua hii muhimu, kama kituo cha televisheni cha taifa ni heshima kubwa kuwaletea michuano hii watazamaji wa TBC. Tunatarajia kufanya kazi kwa ukaribu na KFS Tanzania tukiunganisha mamilioni ya Watanzania watakaokuwa wakitazama michuano hii katika kituo chetu bila malipo yoyote.” Alisema Daphrosa Kimbory, Mkurugenzi wa Masoko TBC.

Meneja Masoko wa KFS Tanzania Gillian Rugumamu pia alikuwa na haya ya kusema kuhusu mchakato huu. “Ikiwa ni channel pekee ya bure ya michezo nchini, KFS Tanzania imejitengenezea wasifu kwa kuzalisha na kurusha vipindi bora zaidi kuanzia vipindi vya hapa nyumbani, vya barani Afrika hadi vya kimataifa vinavyoendana na watazamaji wake.

Ni jambo la furaha kwetu kuleta Kombe la Dunia (FIFA World Cup 2018) pia kwa Watanzania ikiwa ni nyenzo ya kukuza na kuimarisha uhusiano wetu na watazamaji wetu hususani washabiki wa michezo ya kila aina wanaotusogeza karibu kabisa na lengo letu kuu ikiwa ni kuwasilisha burudani kupitia nyenzo mbali mbali ikiwemo kurasa zetu za kijamii kama sehemu ya kusambaza ujumbe wetu wa burudani bure kabisa. Hatua hii imeleta changamoto ambayo haikuwepo katika soko la burudani hapa nchini hususani katika Michuano hii ya Kombe la Dunia.”

“Tuna shauku na furaha kubwa kuwapa Watanzania uwezo wa kuangalia bure michuano hii inayopendwa na kuheshimika kwa umaarufu wake dunia nzima bure kabisa pamoja na chambuzi zake wakiwa majumbani mwao.” Alisema mkurugenzi wa vipindi KFS Tanzania Irene Stanley.

Pamoja na michuano hii, timu ya uzalishaji wa vipindi ya KFS Tanzania wameandaa studio ya aina yake kuelekea kurusha matangazo hayo zitakaporuka preview, highlight na mechi moja kwa moja zitakazochambuliwa na baadhi ya wadau pamoja na watangazaji wa michezo wenye majina na uzoefu katika tasnia hii kwa lugha ya Kiswahili.

Kwa mujibu wa msimamizi mkuu wa eneo hili, Mukhsin Mambo, studio itakuwa ni sehemu kubwa ya mchakato mzima ikishirikisha wakereketwa wa mpira kutoka nyumbani mpaka ughaibuni.

Kwa kupitia ushirikiano huu mahususi wa KFS Tanzania na televisheni ya taifa TBC, watazamaji wanapewa nafasi ya kuungana na mabilioni ya watazamaji kutoka kote duniani kushuhudia michuano hii pasipo kuingia gharama yoyote ukiwa ni mbadala nafuu kwa Mtanzania mwenye kipato cha kawaida.

Kutakuwa na mechi 32, zikiwemo mechi zote zitakazochezwa na timu za Africa, robo fainali, nusu fainali pamoja na mechi ya mwisho ya fainali. Usikose kushuhudia ufunguzi tarehe 14 Juni 2018.

KFS inapatikana kupitia Startimes chanel namba 103, Continental chanel namba 07 pamoja na Ting chanel namba 36.

NA ANDREW CHALE-BONGONEWS

Uongozi ukiwa meza kuu wakati wa tukio hilo la kutiliana saini mkataba wa kuonesha michuano ya Kombe la Dunia kupitia TBC.

Mkurugenzi wa Kwese Free Sports Tanzania (KFS), Joseph Sayi,  akisaini mkataba huo

Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt Ayoub Rioba akisaini mktaba huo

Mkurugenzi wa Kwese Free Sports Tanzania (KFS), Joseph Sayi (kushoto) akiwa na Dkt Ayoub Rioba  wakibadilishana hato za Mktaba huo mara baada ya kusaini wa ushirikiano wa kuonyesha Kombe la Dunia kupitia TBC1..

Mkurugenzi wa Kwese Free Sports Tanzania (KFS), Joseph Sayi (kushoto) akiwa na Dkt Ayoub Rioba  wakionesha mktaba huo mara baada ya kusaini wa ushirikiano wa kuonyesha Kombe la Dunia kupitia TBC1..

Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt Ayoub Rioba.

Mkurugenzi wa Kwese Free Sports Tanzania (KFS), Joseph Sayi,  akiongea na wanahabari katika ofizi za TBC Mikocheni jijini Dar wakati wa tukio.

Wageni kutoka TBC na Kwese free Sports wakifuatilia tukio hilo

Mkurugenzi wa Masoko wa TBC, Bi. Daphrosa Kimbory akizungumza kwenye tukio hilo

Meneja masoko wa TV1, Bi. Gillian Rugamama akizungumza katika tukio hilo

Meneja Mawasiliano wa TBC, Bi.Edna Rajab akizungumza katika tukio hilo

Mtayarishaji wa vipindi na Ubunifu wa TV1, Walter Kimaro akizungumza kwenye tukio hilo

Mtendaji Mkuu wa Kwese tv  Tanzania, Mgope Kiwanga akizungumza kwenye tukio hilo

Tukio hilo likiendelea

Mhariri Mkuu wa Michezo wa TBC, Enock Mbwigane akizungumza kwenye tukio hilo akielezea namna walivyojipanga kutoa radha ya utangazaji wa michezo kwa lugha ya kiswahili wakati wa kombe hilo.

PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE-BongoNews

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here