Benki Kuu yaunganisha Twiga Bancorp na Posta benki

0
101

Serekali kupitia benki kuu ya Tanzania na mmiliki mkubwa wa benki ya Twiga Bancorp imeamua kuiunganisha benki hiyo na benki ya Tanzania posta benki (TPB) ili kuimarisha usimamizi na uendeshaji wake ambapo pia kwa sehemu kubwa inamilikiwa na serekali.

Akizungumza jijini Dar es salaam Naibu Gavana wa benki kuu Benard Kibese amesema kuwa, kwa mamlaka waliyopewa chini ya kifungu cha 30 (1) (a) cha sheria ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2016 wameidhinisha ombi la kuunganisha benki hizo kuanzia Mei 17 mwaka 2018.

Aidha ameongeza kuwa muungano huo utaifanya benki kuu kusitisha usimamizi wa benki ya Twiga na masuala yote ya kuhusu Twiga Bancorp yatafanywa na benki ya TPB ambayo tayari inamtaji wa kutosha kama inavyotakiwa Kisheria.

Hata hivyo benki imewaomba wateja wa benki ya Twiga kuwa watulivu katika kipindi cha uunganishaji wa benki hizo na kuendelea kupata huduma za kibenki kwa utaratibu utakaotolewa na menejimenti ya benki ya TPB.

Ikumbukwe kuwa benki kuu ya Tanzania Oktoba 28 mwaka 2016 iliiweke chini ya usimamizi wake Benki ya Twiga kutokana na kuwa na upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake.

Mary Mtuka

Naibu Gavana wa benki kuu Benard Kibese akizungumza katika tukio hilo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here