Mwakyembe abariki TBC na KWESE Sports kuonesha Kombe la Dunia bure

0
165

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo nchini Dkt. Harrison Mwakyembe, amebariki tukio la ushirikiano baina ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) na KWESE Free Sports Tanznia (KFS) TV One kwa hatua yao ya kuonyesha mechi 32 za Kombe la Dunia kwa bure kabisa mwezi ujao. 

Makyembe ameonesha kufurahishwa na uamuzi wa vituo hivyo vya runinga kuamua kuonesha mashindano hayo yatakayoanza mwezi Juni 2018 huko Russia. 

Aidha, amesema kuwa, jambo hilo ni la kizalendo na linapaswa kuungwa mkono na Watanzania wanaosubiri burudani hiyo kwa hamu kubwa kwani wataishuhudia bure kupitia luninga zao. 

“Nimefuraishwa na uzalendo wa TBC na TV One kwa kuwapatia burudani Watanzani bure. Hiyo itasaidia pia televisheni hizo kujitangaza kimataifa na kupata matangazo” 

Pia amesema: “Hivyo ni fursa kwa Watanzania sasa kupata ya bure kupitia muunganiko wa televisheni hizo mbili za TBC na TV One,” Alieleza. Mwakyembe.

Awali viongozi wakuu wa KWESE Free Sports na TBC walieleza kuwa ushirikiano huo utasaidia kuwasogezea burudani ya mchezo wa soka kwa Watanzania wote hapa nchini ambao watashuhudia bure huku pia wakitangaziwa kwa lugha ya Kiswahili.

Katika tukio hilo wageni mbalimbali walishuhudia akiwemo Balozi wa Urusi, viongozi wa michezo na wasanii mbalimbali akiwemo, msanii Ali Kiba ambaye pia ni balozi wa michuano hiyo.

NA ANDREW CHALE-BONGONEWS

zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali ya tukio hilo la usiku wa Mei 15,2018.

PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE-BONGONEWS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here