SportPesa Super Cup 2018 kufanyika Juni mjini Nairobi, Kenya

0
396

Msimu wa pili wa michuano ya Kombe la SportsPesa Super Cup, kwa mwaka huu wa 2018, inatarajiwa kufanyika kuanzi, 3-10 Juni,2018  Mjini Nairobi Nchini Kenya.

Akizungumza  Afisa Mkuu wa mauzo ya kampuni ya mchezo wa kubahatisha SportPesa, Kelvin Twissa, amesema yanaendelea kupiga hatua na safari hii yatafanyika nchini Kenya huku yakitarajiwa kuboresha uhusiano mzuri kati ya nchi hizo mbili, Tanzania na Kenya.

“Tumechagua timu bora zilizonawiri katika ligi zao Kuu za nyumbani mwaka jana, na pia hii ni njia moja ya kukuza vipaji vya kandanda eneo letu,” alieleza Twissa.

Katika michuano hiyo, Mshindi anapata nafasi ya kusafiri Nchini Uingereza kucheza na  klabu ya Ligi Kuu ya Nchi hiyo ya  Everton katika uwanja wao wa Goodison Park.

Mpaka sasa Bingwa mtetezi wa kombe hilo ni Gor Mahia ambaye alitwaa kombe hilo lilipofanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.

Kiasi cha dola 57,500 zitashindaniwa katika mashindano hayo ya wiki moja yatakayofanyika katika uwanja wa Kasarani.

Timu za Kenya ni pamoja na Gor Mahia, AFC Leopards, Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboyz kwa upande wa miamba ya Tanzania ni pamoja na Bingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara 2017/2018 Simba SC,Yanga,  Singida FC na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) ya Zanzibar.

Msimu uliopita:

Katika mechi za robo-fainali, AFC Leopards ilishinda Singida FC kwa mabao 5-4 ya penalti baada ya sare ya bao 1-1, Yanga ikashinda Tusker ya Kenya mabao 4-2 ya penalti kutokana na sare tasa, Gor Mahia ikainyoa Jang’ombe 2-0 na Simba ikakatwa mkia na Nakuru All Stars ya Kenya kwa kumeza mabao 5-4 ya penalti kutokana na sare tasa.

Matumaini ya Nakuru All Stars kusonga mbele yalifikia kikomo mechi za nusu fainali ilipolimwa mabao 2-0 na Gor Mahia, huku Leopards ikiing’oa Yanga kwa mabao 4-2 ya penalti baada ya sare ya kutofungana. Katika mechi ya fainali Gor Mahia ilizima kidomodomo cha Leopards kwa mabao 3-0.

Na Andrew CHALE-BongoNews

Afisa Mkuu wa mauzo ya kampuni ya mchezo wa kubahatisha SportPesa, Kelvin Twissa akizungumza katika tukio hilo leo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here