MultiChoice Tanzania yatunukiwa tuzo na Serikali

0
89

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wametoa tuzo maalum kwa Kampuni ya MultiChoice Tanzania inayosambaza vifaa vya DSTV hapa nchini, kwa kutambua mchango mkubwa wa kampuni hiyo katika sekta ya filamu hapa nchini.

Tukio hilo limefanyika mwishoni mwa wiki  wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania iliyofanyika Jijini huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harison Mwakyembe.

Tukio hilo pia limeshuhudiwa na wadau mbalimbali wa filamu nchini pamoja na viongozi waandamizi wakiwemo Katibu Mkuu Wizara Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Suzan Mlawi na Mwenyekiti mpya wa Bodi ya filamu  Prof. Frowin Nyoni.

Hivi karibuni MultiChoice Tanzania iliweza kuzindua program maalum  ijulikanao kama MultiChoice Talent Factory (MTF) ambayo itakuwa inalenga kuchochea ubunifu  wa vijana wa Afrika katika tasnia ya filamu ambao watakuwa wakipata ufadhili wa kusomea fani hiyo katika vyuo vikuu vya filamu Barani Afrika.

Na Andrew Chale-BongoNews

Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harison Mwakyembe akimkabidhi Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana tuzo maalum iliyotolewa na Bodi ya Filamu Tanzania kutambua mchango mkubwa wa kampuni hiyo katika sekta ya filamu hapa nchini. Hiyo ilikuwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Ushauri ya Bodi ya Filamu Tanzania iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. wanaoshuhudia ni Katibu Mkuu Wizara Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Suzan Mlawi na mwenyekiti mpya wa bodi hiyo Prof. Frowin Nyoni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here