Samia awataka viongozi ngazi zote kuongeza nguvu utunzaji Mazingira

0
175

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa ngazi zote kuongeza nguvu katika utekelezaji wa  Sera, Sheria, Mikakati na miongozo katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

Makamu wa Rais  ameyasema hayo wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Dar es Salaam kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja.

“ Ni muhimu, mipango ya maendeleo katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira ili nchi yetu iwe na maendeleo endelevu”alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amesema kazi ya kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa hifadhi ya mazingira unahitaji ushirikiano wa wadau wote kwa ngazi zote.

Maadhimisho ya Kimataifa yanafanyika  India  katika mji wa New Delhi ya kibeba ujumbe wa kuhimiza kupunguza uchafuzi wa mazingira kutokana na matumizi ya bidhaa za plastiki (Beat Plastic Pollution) lakini hapa nchini Kitaifa ujumbe wa maadhimisho ni “Mkaa Gharama: Tumia Nishati Mbadala”

Mapemaleo, Makamu wa Rais alizindua ukuta wa bahari uliopo kwenye barabara ya  Barack Obama  wenye urefu wa mita 920, ukuta huo ambao umejengwa kuzuia bahari kuingia nchi kavu unakadiriwa kuwa na maisha kati ya miaka 70 mpaka 100 kutoka sasa.

Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga uchumi wa Viwanda na zipo faida nyingi za hifadhi na usimamizi zitakazotokana na  Tanzania kuwa na Viwanda.

Mwisho, Makamu wa Rais amesema katika kufanikisha suala zima  la uhifadhi wa Utunzaji wa mazingira ni lazima tuifanye kila siku iwe siku ya Mazingira.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Bw. Leonard Kushoka mfano wa hundi yenye thamani ya shiliningi za kitanzania milioni 300 mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano la teknolojia ya nishati mbadala wa mkaa mwaka 2018, wengine pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na Mwenyekiti Mkazi wa Kampuni ya Shell Bw. Axel Knospe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here