Rais Magufuli amteua Bw. Athuman Selemani Mbuttuka kuwa Msajili wa Hazina

0
192

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Athumani Selemani Mbuttuka kuwa Msajili wa Hazina (Treasury Registrar).

Uteuzi wa Bw. Mbuttuka umeanza leo tarehe 06 Juni, 2018.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Mbuttuka alikuwa Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Taifa (DAG) katika Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (NAOT).

Bw. Mbuttuka anachukua nafasi ya Dkt. Oswald Mashindano ambaye amestaafu.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

06 Juni, 2018

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here