WILAYA 93 zafanikiwa kutokomeza Matende na Mabusha Nchini

0
76

WILAYA 93 nchini yafanikiwa kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yakiwemo matende na mabusha ambapo wilaya hizo awali zilikua zikihitaji kingatiba ila kwa sasa hazihitaji .

Hayo yamesemwa na Katibu mkuu Wizara ya afya Dkt. Mpoki Ulisubisya katika uzinduzi wa mkutano wa kujadili, kupitia na kupanga utekelezaji wa mpango kazi katika kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele jijini Dar es salaam.

“Tumetoa dawa kwa watanzania wapatao milioni 21 kati ya milioni 50 hivyo kupiga hatua kubwa katika kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele hapa nchini kwetu” alisema Dkt. Ulisubisya.

“Tumetoa dawa kwa Watanzania wapatao Milioni 21 Kati ya Milioni 50 hivyo kupiga hatua kubwa katika kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele hapa nchini kwetu.

Hao milioni  21 ni ambao hawahitaji tena kinga tiba kwa sasa kutokana na kufanikiwa kukingwa na maambukizi huku ikiwa dawa tunatoa bado watu milioni 29 wanaendelea kupewa.” Ameeleza

Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa mkutano huo uliokutanisha wadau wa afya wa nje na ndani ya nchini unalenga kutoka na mkakati wa kupambana na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele hasa maeneo ya vijijini.

Kwa upande wake Mratibu wa Taifa wa mpango wa kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchini Dkt. Upendo Mwingira amesema kuwa wananchi wanatakiwa wajitokeze kwenye mazoezi ya kupata dawa za kuzuia mabusha na matende.

“Tunatakiwa kujitokeza kila mwaka mara pindi itakapotangazwa kuwa ni kipindi cha kupata dawa hizo na mwaka huu dawa hizo zitatolewa Septemba kwa watanzania wote” alisema Dkt. Mwingira.

Aidha Dkt. Mwingira amesema kuwa mbali na mafanikio yaliyopatikana katika kampeni hiyo ya kutokomeza magonjwa hayo pia kuna changamoto za utoaji elimu na uhamasishaji katika matumizi ya dawa hizo.

Hata hivyo amesema kwa upande wa ugonjwa wa Vikope(Trakoma) wamefanikiwa kusitisha kugawa dawa kwa wilaya 58 kati ya 71 nchini.
Mbali na hayo Dkt. Mwingira amesema kuwa katika kuhakikisha magonjwa hayo yanapotea nchini wamejidhatiti kuzindua kampeni ya kuwafanyia upasuaji watu 350 Kisarawe Mkoani Pwani.

Mkutano huo ni wa siku tatu huku washiriki wake wakitoka mataifa  mbalimbali

Katibu mkuu Wizara ya afya Dkt. Mpoki Ulisubisya akiwasili kwenye uzinduzi wa mkutano wa kujadili, kupitia na kupanga utekelezaji wa mpango kazi katika kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ulioanza leo Juni 6,2018 jijini Dar es salaam.

Meza kuu katika tukio hilo

Katibu mkuu Wizara ya afya Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkutano wa kujadili, kupitia na kupanga utekelezaji wa mpango kazi katika kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ulioanza leo Juni 6,2018 jijini Dar es salaam.

Washiriki wakifuatilia tukio hilo

Katibu mkuu Wizara ya afya Dkt. Mpoki Ulisubisya akifungua rasmi mkutano wa kujadili, kupitia na kupanga utekelezaji wa mpango kazi katika kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ulioanza leo Juni 6,2018 jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa NIMRProf. Yunus Mgaya akizungumza katika tukio hilo

Katibu mkuu Wizara ya afya Dkt. Mpoki Ulisubisya akiwa katika picha ya pamoja washiriki wa  mkutano  huo wa kujadili, kupitia na kupanga utekelezaji wa mpango kazi katika kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ulioanza leo Juni 6,2018 jijini Dar es salaam.

Katibu mkuu Wizara ya afya Dkt. Mpoki Ulisubisya akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa walioandaa mkutano wa kujadili, kupitia na kupanga utekelezaji wa mpango kazi katika kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ulioanza leo Juni 6,2018 jijini Dar es salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here