Tamasha la Sports Music Festval 2018 kufanyika mikoa mitatu Kanda ya Ziwa

0
148

Tamasha kubwa na la aina yake la Sports Music Festival 2018 linatarajiwa kurindika katika Mikoa mitatu  ya Kanda ya Ziwa  kwa mara ya kwanza huku ikitarajiwa kuwa na Wasanii nyota Nchini pamoja na michezo mbalimbakli ikiwemo mbio za magari na Pikipiki kwenye mikoa ya Geita, Kahama-(Mkoa wa Shinyanga) na Mwanza.

Akizungumza na wanahabari mapema leo Jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko  na waandaaji wa tamasha hilo, Eberhard  Osward ‘Ebe  Nation’ ameeleza kuwa, tayari mipango yote imekamilika na tayari Wasanii na  wanamichezo wakiwemo waendesha magari na pikipiki wamesha wasili Kanda ya Ziwa.

“Tayari, Wanamichezo wapo Kanda ya Ziwa kuangalia njia watakazotumia. Hii ni kwa yale mashindano ya Magari na Pikipiki. Pia wasanii  baadhi yao na wengine wanaanza kuwasili Kanda ya Ziwa kesho.

tamasha ili linafanyika kwa mara ya kwanza kwa kuandaliwa na Pesasina kwa ushirikiano na Isbah Entertainment hii ni kama zawadi maalum kwa wakazi wa kanda ya Ziwa na litafanyika katika kusherehekea sikuku ya Idd”Alieleza Ebe Nation.

Aidha, Ebe Nation amewataja baadhi ya Wasanii hao watakao tumbuiza siku hizo ni Mbunge wa Mikumi Profesa Jay, Juma Nature, Young Killer, Roma, Stamina, Fid Q, Bill Nas, Umber Lulu.

Pia wapo wasanii Snura, Msaga Sumu, G Nako, Young Dee, Coyo Mc, Fany, B-Gwai pamoja na mkali wa singeli Shalo Mwamba.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Sports Music, Sharon Sudi amesema kuwa kiingilio kimezingatiwa kwa gharama ya chini kabisa.

“Siku ya Idd Mosi wataanzia Geita katika viwanjwa vya Infotech ambapo kiingilio kwa wakubwa ni shilingi 5000 na watoto ni 3000.

Idd Pili watatapiga hodi Mkoani Mwanza katika viwanja vya CCM kirumba, na baada ya hapo watamalizia burudani Mjini Kahama pale Uwanja wa Taifa kwa kiingilio cha Shilingi  10000 wakubwa, huki watoto wakilipia mlangoni 5000.

Tamasha  hilo  litaanza saa 4 asubuhi mpaka majogoo ambapo pia watashuhudia michezo ya piki piki na magari yakifanya maajabu yake ya dunia” Amemalizia  Sharon Sudi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here