RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA AMESEMA KUA KENYA WATAKUA KATIKA MAOMBOLEZO YA SIKU 3 BAADA YA KIFO CHA RAIS MSTAAFU BENJAMIN WILLIAM MKAPA

Marehemu Rias Benjamin William mkapa

Alikua na mchango mkubwa sana katika kupigiania uchanguzi wa Kenya mwaka 2008 hivyo basi wakenya wote watakua katika maombolezo ya siku tatu 

Watu mbali mbali wametoa salamu za rambi rambi kwa Rais wa Tanzania kifo cha Rais mstaafu 

Rais John Pombe Magufuli alitangaza usiku wa kuamkia leo Ijumaa kupitia runinga ya taifa taarifa za kuaga dunia kwa kiongozi huyo wa awamu ya tatu katika hospitali moja jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Rais Magufuli alisema Bw. Mkapa amekuwa akipokea matibabu katika hospitali moja jiji Dar es Salaam, na kuongeza kuwa maelezo zaidi yatatolewa baadae.

”Mzee Benjamin William Mkapa Rais wa awamu ya tatu amefariki. Amefariki kwenye hospitali mjini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa. Niwaombe watanzania tulipokee hili. Taifa limepata msiba mkubwa. Tuendelee kumuombea Mzee wetu Rais Benjamin William Mkapa ambaye ametangulia mbele ya haki,” ametangaza rais Magufuli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *