KITAIFA

MATUMAINI MAKUBWA BANDARI YA MTWARA, RAIS SAMIA ATAAKA BIDII, WELEDI NA UADILIFU

MATUMAINI MAKUBWA BANDARI YA MTWARA, RAIS SAMIA ATAAKA BIDII, WELEDI NA UADILIFU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema takwimu alizopata zinaonyesha bandari ya Mtwara inaweza kuwa ya pili kwa ukubwa ukiachana na bandari ya Dar es Salaam kama watendaji wake watafanya kazi kwa bidii, weledi na uadilifu ili kuvutia wafanyabiashara zaidi.

Rais Samia ameyasema hayo leo Septemba 15, 2023 alipotembelea Bandari ya Mtwara kukagua ufanyaji kazi wake na maendeleo ya bandari hiyo.

“Bandari hii imejengwa kwa kuifungua Mikoa ya kusini kupitia Mtwara bandari hii tunategemea itoe huduma kwa mikoa jirani kwahiyo uchapa kazi wenu ndo utavutia biashara nyingi kuja kwenye bandari hii.” amesema Rais Samia.

Aidha Dkt. Samia amesema kwa upande wa serikali wanajitahidi kutenga bajeti ya kuboresha miundo mbinu ya bandari ili huduma zaidi zitolewe na kuvutia wafanyabiashara kutumia bandari ya Mtwara.

Hata hivyo amesema serikali inajitayarisha kusafirisha korosho kupitia bandari ya Mtwara hivyo wannachi waendelee kujipanga vizuri na kuiunga serikali mkono ili waingize mapato zaidi.

About Author

Bongo News

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *