KITAIFA

WAZIRI MKUU: TUNATAKA KILA MWANANCHI APATE KITAMBULISHO CHA TAIFA

WAZIRI MKUU: TUNATAKA KILA MWANANCHI APATE KITAMBULISHO CHA TAIFA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mkakati wa Serikali ni kumwezesha kila Mtanzania apate kitambulisho cha Taifa akiwa kijijini kwake.

Amesema hayo leo (Alhamisi, Mei 11, 2023) bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Biharamulo Magharibi, Mhandisi Ezra Chiwelesa kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu. 

Mbunge huyo alitaka kujua ni kwa nini Serikali haioni haja ya kuanza mchakato wa kuhuisha vitambulisho vya Taifa kama ilivyofanya kwenye zoezi la awali kwa kuwa kuna vijana wengi ambao wamefikisha umri wa miaka 18 na hawakupata fursa ya kujiandikisha kwenye awamu ya kwanza kwa hiyo hawana vitambulisho hivyo kama sera inavyotaka ikiwemo wananchi wa mikoa ya pembezoni.

Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea na zoezi la utoaji wa vitambulisho kupitia taasisi ya NIDA ambayo awali ilikuwa na changamoto ya upungufu wa watumishi lakini hivi sasa imeshatatuliwa. “Awali tulikuwa na idadi ndogo sana ya watumishi wa kuweza kuwafikia wananchi. Kwa sasa tumeongeza idadi ya watumishi na ninamshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa kuipongeza Serikali kwani vitambulisho vinatolewa kwa wingi.” 

Waziri Mkuu amesema alishafanya ziara katika mikoa ya Kigoma, Kagera na Arusha (wilaya za Biharamulo na Longido) akakuta kuna changamoto ya upatikanaji wa vitambulisho hivyo kwa sababu kasi ya utoaji ni ndogo. “Inawezekana kabisa wale ambao hawajafikiwa na hasa kwenye mikoa ya pembezoni, ni kutokana na kuwepo kwa changamoto ya muingiliano wa mataifa ya jirani. Kitambulisho hiki ni cha Taifa, na kinahusu usalama wa Taifa letu, tusingependa asiye raia awe nacho kwa sababu kitambulisho hiki ni mali ya Watanzania. Ndiyo maana, kwenye maeneo ya mpakani umakini unaongezeka.”

Waziri Mkuu amesema Serikali itawafikia wananchi zaidi kwa kuwapatia vitambulisho na wale ambao bado hawajapata, itawapatia namba za vitambulisho ili wazitumie kwenye mahitaji yao wakati wakisubiri vitambulisho hivyo.

About Author

Bongo News

4 Comments

    I not to mention my buddies were found to be checking the good pointers from the website while then I got an awful feeling I never expressed respect to the site owner for those techniques. My boys came so joyful to study them and have now without a doubt been taking advantage of them. Appreciate your getting very kind as well as for picking this kind of marvelous guides most people are really desperate to learn about. Our own honest apologies for not expressing gratitude to you sooner.

    Utterly pent subject matter, thank you for information. “Life is God’s novel. Let him write it.” by Isaac Bashevis Singer.

    He never apologies buy priligy without a script Hepatomegaly, Elevated Serum liver enzymes Low HDL Hypercholesterolemia Fatty liver on ultrasound

    Many geriatricians consider it more problematic than the classic Schedule II opiates listed above, as it interacts with a lot of medications and still affects brain function how to buy generic cytotec Using the cube model approach, the panel identified, by consensus, limits between high, moderate and low load

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *