Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu
akiongoza kikao cha pamoja na kati ya Wizara na ujumbe kutoka Chama cha Mapinduzi
(CCM) kilichofanyika Juni 16, 2023 jijini Dodoma ambapo wamejadili namna bora ya
kuboresha miundombinu ya michezo nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amekutana na kufanya kikao cha pamoja na ujumbe kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo wamejadili namna bora ya kuboresha miundombinu ya michezo nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu
akiongoza kikao cha pamoja na kati ya Wizara na ujumbe kutoka Chama cha Mapinduzi
(CCM) kilichofanyika Juni 16, 2023 jijini Dodoma ambapo wamejadili namna bora ya
kuboresha miundombinu ya michezo nchini.
Kikao hicho kimefanyika Juni 16, 2023 jijini Dodoma ambapo timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiongozwa na Katibu Mkuu wake Bw. Saidi Yakubu na ujumbe wa CCM ukiongozwa na Bw. Mussa Matoroka MNEC na Katibu wa CCM mkoa wa Arusha.
Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili kuhusu uendeshaji na usimamizi wa viwanja vya michezo vinavyomilikiwa na kusimamiwa na Serikali pamoja na CCM ambavyo vinatumika katika michezo mbalimbali nchini ikiwemo Ligi Kuu ya NBC.
Kiongozi wa ujumbe wa Chama Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni MNEC Bw.
Mussa Matoroka akichangia hoja wakati wa kikao kilichofanyika Juni 16, 2023 jijini
Dodoma ambapo wamejadili namna bora ya kuboresha miundombinu ya michezo
inayosimamiwa nchini.
Kikao hicho kimehudhuriwa wajumbe nane kutoka CCM akiwemo Mhasibu Mkuu wa CCM Taifa Bw. Thobias Abwalo huku ujumbe wa Wizara yenye dhamana na michezo ikiwa na wajumbe saba akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini Bw. Ally Mayayi.