KITAIFA

WAZIRI KAIRUKI AISHUKURU TAASISI YA UTAFITI WA KIMATAIFA MATIBABU YA HENRY JACKSON KWA KUCHANGIA MAPAMBANO DHIDI YA VVU/UKIMWI

WAZIRI KAIRUKI AISHUKURU TAASISI YA UTAFITI WA KIMATAIFA MATIBABU YA HENRY JACKSON KWA KUCHANGIA MAPAMBANO DHIDI YA VVU/UKIMWI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Angellah Kairuki akizungumza na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kimataifa wa Matibabu ya Henry Jackson, Meja Generali Mstaafu Dkt. Joseph Caravalho ambaye taasisi yake inatoa mchango katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU na UKIMWI.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Mhe. Angellah Kairuki ameishukuru Taasisi ya Utafiti wa
Kimataifa wa Matibabu ya Henry Jackson (Henry Jackson Foundation for
Medical Research International) kwa kuunga mkono jitihada za Serikali
ya Awamu ya Sita katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya
Ukimwi (VVU) na UKIMWI.
Mhe. Kairuki ametoa pongezi hizo kwa Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa
Taasisi ya Utafiti wa Kimataifa wa Matibabu ya Henry Jackson, Meja
Generali Mstaafu Dkt. Joseph Caravalho aliyemtembelea ofisini kwake
Jijini Dodoma Leo.
Mhe. Kairuki amesema, Taasisi ya Utafiti wa Kimataifa wa Matibabu ya
Henry Jackson imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Tanzania
inadhibiti janga la UKIMWI kupitia kinga, matunzo, matibabu ya VVU na
utoaji wa msaada kwa watu wanaoishi na VVU.

Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kimataifa wa Matibabu ya Henry Jackson, Meja Generali Mstaafu Dkt. Joseph Caravalho (wa kwanza kulia) na watendaji wengine wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Angellah Kairuki (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha viongozi hao.


Mhe. Kairuki amefafanua kuwa, taasisi hiyo ya utafiti maarufu kama Walter
Reed Program imekuwa ikifanya kazi kwa miaka mingi tangu mwaka 2004
akitoa mfano kwenye mikoa ya nyanda za juu kusini ambayo ni Mbeya,
Songwe, Rukwa, Katavi na Ruvuma ambapo taasisi hiyo imeshirikiana
vema na Ofisi ya Rais-TAMISEMI pamoja na Wizara ya Afya.
Naye, Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kimataifa wa
Matibabu ya Henry Jackson, Meja Generali Mstaafu wa Jeshi la Marekani
Dkt. Joseph Caravalho ameishukuru Serikali ya Tanzania chini ya uongozi
makini wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan ambaye amekuwa ni kinara wa kujenga mahusiano ya
kidplomasia yaliyoiwezesha taasisi yake kutoa mchango katika eneo la
mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *