KITAIFA

SERIKALI KUIMARISHA MIKAKATI KUKABILI MAAFA

SERIKALI KUIMARISHA MIKAKATI KUKABILI MAAFA

Picha ya pamoja wakati wa kikao kazi cha wataalam waliokutana kwa lengo la kufanya Tathimini ya uwezo wa Kukabiliana na Maafa kilichofanyika Jijini Dodoma.

SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu imesema inaendelea kuboresha mikakati ya kukabiliana na maafa ili kuhakikisha wananchi wanaishi katika hali ya usalama.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Utafiti wa Maafa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Charles Msangi wakati akifungua  kikao  kazi  cha  wataalam waliokutana kwa lengo la kufanya Tathimini ya uwezo wa Kukabiliana na Maafa kilichofanyika Jijini Dodoma.

Naibu Mkurugenzi Mkaazi kutoka WFP Bw. Brian Bogart akifafanua jambo katika kikao hicho.

Amesema Nchi imepiga hatua kubwa katika kukabiliana na maafa kutokana na kuimarisha mfumo wa utendaji kwa kutunga Sheria ya Usimamizi wa Maafa, Na. 6 ya mwaka 2022 na Kanuni zake za mwaka 2022 pamoja na kuimarisha mifumo ya tahadhari ya mapema, kuimarisha miundombinu, vifaa na miongozo kwa ajili ya kukabilina na maafa na kurejesha hali.

“Nchi yetu  imepiga hatua katika kutekeleza Mkakati wa Sendai kwa kuweka mazingira ya uwekezaji katika kupunguza vihatarishi vya maafa kwa kuandaa Mkakati wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa (2022-2027) pamoja miongozo, mipango na mikakati ya kitaifa na kisekta,”Amesema Bw. Msangi.

Baadhi ya watalaam kutoka Wizara mbalimbali, Taasisi na Mashirika wakifuatilia kikazo  kazi  cha wataalam waliokutana kwa lengo la kufanya Tathimini ya uwezo wa Kukabiliana na Maafa kilichofanyika Jijini Dodoma.

Pia ameongeza kuwa kila sekta inapaswa kuwa imara katika eneo lake ili kuepuka madhara kwa kuzingatia maeneo ya vipaumbele kulingana na uwezo uliopo sasa wa kukabiliana na maafa hivyo akawasisitiza wataalam kuzielewa sekta zao katika usimamizi wa maafa kabla ya kuchukua hatua yoyote.

“Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa iliratibu zoezi la tathmini ya uwezo wa udhibiti wa maafa kupitia jumuiya ya ushirikiano inayotambulika kama Capacity for Disaster Reduction lnitiative (CADRI) inayojumuisha Mashirika 20 ya Umoja wa Mataifa na Kimataifa yanayotoa huduma za kibinadamu na kutekeleza shughuli za maendeleo,”Ameeleza.

Baadhi ya watalaam kutoka Wizara mbalimbali, Taasisi na Mashirika wakifuatilia kikazo  kazi  cha wataalam waliokutana kwa lengo la kufanya Tathimini ya uwezo wa Kukabiliana na Maafa kilichofanyika Jijini Dodoma.

Aidha ikumbukwe Tathmini ilifanyika tarehe 17 hadi 28 Octoba, 2022, ikilenga kutambua hali ya uwezo uliopo na maeneo ambayo Mashirika husika yanaweza kushirikiana na Serikali kuimarisha udhibiti wa maafa nchini.

Naye Naibu Mkurugenzi Mkaazi kutoka WFP Bw. Brian Bogart ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na shirika hilo ili kuhakikisha raia wake wanashiriki katika shughuli za maendeleo wakiwa katika mazingira rafiki.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *