Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu (wa nne
kulia) na Balozi wa Urusi nchini Mhe. Andrey Avetisyan (wa tatu kushoto) wakiwa
kwenye picha ya Pamoja mara baada ya kikao kikao chao Juni 21, 2023 jijini Dar es
Salaam ambapo wamejadili namna bora ya Tanzania na Urusi kushirikiana katika sekta
ya Utamaduni na Sanaa kwa manufaa wa wananchi wa pande hizo mbili.
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Urusi nchini Mhe. Andrey Avetisyan ambapo wamejadili namna bora ya Tanzania na Urusi kushirikiana katika sekta ya Utamaduni na Sanaa kwa manufaa wa wananchi wa pande hizo mbili.
Akiongea wakati wa kikao hicho kilichofanyika Juni 21, 2023, Katibu Mkuu Bw. Yakubu amesema Tanzania na Urusi wataendelea kushirikiana katika eneo la Utamaduni na Sanaa kwa kuzingatia uhusiano wa muda mrefu ulipo baina nchi hizo mbili katika masuala mbalimbali ikiwemo lugha ya Kiswahili.
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akiwa
kwenye kikao Juni 21, 2023 jijini Dar es Salaam na Balozi wa Urusi nchini Mhe. Andrey
Avetisyan ambapo wamejadili namna bora ya Tanzania na Urusi kushirikiana katika
sekta ya Utamaduni na Sanaa kwa manufaa wa wananchi wa pande hizo mbili.
“Tunatambua juhudi zinazofanywa nan chi ya Urusi kwa kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili, sisi tupo tayari kupitia BAKITA kutoa vitabu vya kujifunzia Kiswahili, tutatoa vitabu kwa walimu wa Kiswahili kutoka Urusi ambao watakuja hapa nchini wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani Julai 7 mwaka huu ili vitabu hivyo viwe nyenzo nzuri ya kufundishia lugha ya Kiswahili Urusi” amesema Bw. Yakubu.
Kwa upande wake Balozi wa Urusi nchini Mhe. Andrey Avetisyan amesema nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika Nyanja mbalimbali za maendeleo ambapo wataendelea kutoa nafasi kwa Watanzania kusoma nchini humo ambapo watajifunza pia lugha ya Kirusi ili kuendeleza mahusiano ya kibiashara na uchumi hatua inayoongeza nafasi kwa Watanzania kufanya kazi Urusi na Warusi kufanya kazi Tanzania.
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akiwa
kwenye kikao Juni 21, 2023 jijini Dar es Salaam na Balozi wa Urusi nchini Mhe. Andrey
Avetisyan ambapo wamejadili namna bora ya Tanzania na Urusi kushirikiana katika
sekta ya Utamaduni na Sanaa kwa manufaa wa wananchi wa pande hizo mbili.
Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Bi. Consolata Mushi amesema watashirikiana na Ubalozi wa Urusi nchini ambapo wafundisha maafisa wa Ubalozi huo lugha ya Kiswahili kwa wageni na watashirikiana nao kufundisha wataalam wa tafsiri na ukalimani hatua itakayosaidia kueneza lugha ya Kiswahili duniani.
1 Comment
Do I have another cataract emla cream and priligy tablets It is very important to continue giving this medication and other HIV medications exactly as prescribed by the doctor