KITAIFA

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya
uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkaguzi Mkuu wa
Ndani wa Serikali kama ifuatavyo:
1) Amemteua Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Mbarouk Salim
Mbarouk kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Jaji
Mstaafu Mbarouk ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kipindi cha pili.
2) Amemteua Mhe. Balozi Omar Ramadhan Mapuri kuwa Mjumbe wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi. Mhe. Balozi Mapuri ameteuliwa kuwa Mjumbe kwa kipindi
cha pili.
3) Amemteua Dkt. Zakia Mohamed Abubakar kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi.
Uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi unaanza tarehe 01 Julai, 2023.
4) Amemteua Prof. Idrissa Mshoro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya
Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA). Prof. Mshoro ameteuliwa kuwa
Mwenyekiti wa Bodi kwa kipindi cha pili.
5) Amemteua Bw. Benjamin Mashauri Magai kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa
Serikali. Kabla ya uteuzi Bw. Magai alikuwa Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali.
Uteuzi huu umeanza tarehe 25 Juni, 2023.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *