KITAIFA

DKT. MSONDE AWATAKA WALIMU KUWAPATIA WATOTO MALEZI BORA NA UJUZI

DKT. MSONDE AWATAKA WALIMU KUWAPATIA WATOTO MALEZI BORA NA UJUZI

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde akitoa maelekezo mara baada ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya elimu katika shule ya sekondari Mwanzi iliyopo wilayani manyoni.

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa Dkt. Charles Msonde amewataka walimu wa elimu ya awali
kuhakikisha wanawapatia watoto malezi bora na ujuzi ili wakianza darasa
la kwanza wawe na msingi mzuri wa elimu.

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde akizungumza na Walimu, Maafisa Elimu Kata na Walimu Wakuu wa Mkoa wa Singida wakati akifungua mafunzo yanayolenga kuwawezesha kutoa elimu yenye tija kwa watoto.


Dkt. Msonde ametoa wito huo kwa walimu wote shule za awali nchini,
wakati akifungua mafunzo ya walimu 105, Maafisa Elimu Kata 21 na
Walimu Wakuu 21 wa Mkoa wa Singida ambayo yatakayowawezesha
kutoa elimu yenye tija kwa watoto.
Dkt. Msonde amesema, Serikali inathamini elimu ya awali na ndio maana
kupitia mradi wa BOOST madarasa ya awali 12,000 yatajengwa ili
kuwezesha shule zote za msingi nchini kuwa na madarasa ya awali kwani
miongoni mwa shule zote takribani 17,000 zilizopo baadhi yake tayari zina
madarasa ya awali.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Manyoni, Mwalimu James Mchembe akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde kuzungumza na Walimu, Maafisa Elimu Kata na Walimu Wakuu wa Mkoa wa Singida walioudhuria mafunzo yatakayowezesha kutoa elimu yenye tija kwa watoto.


“Elimu ya awali inajenga msingi bora wa malezi ya mtoto, tabia nzuri,
pamoja na utamaduni wa mtoto kupenda shule, na ndio maana Mhe. Rais
aliridhia mradi wa BOOST utengewe trilioni 1.15 kwa ajili ya kuboresha
miundombinu ya elimu katika kipindi cha miaka 5 cha utekelezaji wa mradi
huo,” Dkt. Msonde amefafanua.

Sehemu ya na Walimu, Maafisa Elimu Kata na Walimu Wakuu wa Mkoa wa Singida wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo yanayolenga kuwawezesha watendaji hao kutoa elimu yenye tija kwa watoto.


Ameongeza kuwa, mradi huo umetoa fursa kwa walimu hao kujengewa
uwezo wa kutoa mafunzo kwa watoto kwa kulingana na hatua za makuzi.
Kwa upande wake, kiongozi wa wawezeshaji, Dkt. Fortunata Pembe
amesema, pindi walimu hao wakihitimu mafunzo hayo watakuwa tayari
kutoa mafunzo kwa walimu wengine.

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa elimu ya awali wanaoshiriki mafunzo yanayolenga kuwawezesha walimu hao kutoa elimu yenye tija kwa watoto.

Naye, Mwalimu Kitila Mkumbo ambaye ni miongoni mwa washiriki wa
mafunzo hayo, ameshukuru kwa kupatiwa mafunzo na kuahidi kuyatumia
vizuri ili watoto wapate malezi bora na ujuzi.

About Author

Bongo News

1 Comment

    Транснациональные перевозки играет важнейшую задачу в организации ввоза продукции в Россию. Это сложный процесс, включающий логистическую координацию, таможенное оформление и оптимизацию логистики. Грамотная стратегия и выбор надежных партнеров обеспечивают безопасность и способствуют успешной доставке.

    Одной из важнейших целей в грузоперевозках является выбор вида транспорта – https://ved-mezhdunarodnaya-logistika.ru/ . Для грузоперевозок на территорию РФ используются разные маршруты: морские перевозки экономически эффективны, авиатранспортировка — груза высокой стоимости, а наземный транспорт — для баланса скорости и цены. Территориальные особенности нередко требует комбинированные маршруты.

    Не менее ключевой частью является таможенная очистка. Профессиональный подход к таможенным требованиям, соблюдение законодательства и знание ограничений помогают избежать задержек. Работа с профессионалами позволяет учитывать особенности, что критично для результата.

    Цифровые решения активно изменяют международную логистику. Трекеры грузов, системы складского учета и аналитические платформы улучшают эффективность поставок. Это позволяет бизнесу реагировать на вызовы, адаптироваться к требованиям и поддерживать бесперебойные поставки.

    Глобальные перевозки зависит от грамотного управления, профессионализма и налаженных отношений. Это главное звено, позволяющий компаниям в России развивать свои процессы и строить глобальные связи.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *