BURUDANI

NCHI ZAIDI YA 20 ZASHIRIKI TAMASHA LA ZIFF MJINI ZANZIBAR

NCHI ZAIDI YA 20 ZASHIRIKI TAMASHA LA ZIFF MJINI ZANZIBAR

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akikabidhi
tuzo ya filamu kwa mmoja wa washindi wa tuzo hizo wa Tanzania wakati wa kufunga Tamasha la 26 la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) Julai 02, 2023 mjini Zanzibar.

Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) limehitimishwa ambapo nchi zaidi ya
20 zimeshiriki ikiwemo wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi,
Cameroon, Qatar, Congo DRC, Misri, Algeria, Tunisia, Morocco, Italy, Israel, Ufaransa,
Uingereza, Ireland, Afghanistan, Denmark, Hispania, Angola, Namibia, Afrika Kusini,
China, Zambia, Zimbabwe na Uswizi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hamza Hassan
Juma akifunga Tamasha la 26 la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) Julai 02, 2023
mjini Zanzibar.

Tamasha hilo limehitimishwa Julai 2, 2023 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma ambaye alitoa tuzo kwa filamu bora na ndefu ya kisayansi (Sci-Fi) ya EONII iliyozinduliwa hivi karibuni jijini Dar es salaam

Tamasha hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya
Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu, Dkt. Kilonzo Kiagho ni miongoni mwa
wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani kutoka mataifa hayo.

Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla ya kufunga Tamasha la 26 la
Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) Julai 02, 2023 mjini Zanzibar.

Ni mwaka wa 26 tangu Tamasha la ZIFF lilipoanzishwa mwaka wa 1997 kuendeleza na
kukuza tasnia ya filamu na mambo mengine ya kiutamaduni kama kichocheo cha ukuaji wa kijamii na kiuchumi wa kikanda.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *