Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa Ilemela mkoani Mwanza wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika jimbo lake jana.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameagiza kuwepo usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika jimbo la Ilemela mkoani Mwanza.
Dkt Mabula ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela alisema hayo jana tarehe 4 Julai 2023 jijini Mwanza akiwa katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula akisalimiana na viongozi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Ilemela mkoa wa Mwanza wakati wa ziara ya kagua miradi ya maendeleo jimbo la Ilemela jana.
Katika ukaguzi huo, Waziri Mabula alisisitiza pia umuhimu wa matumizi thabiti ya fedha za Maendeleo sambamba na Uzalendo wakati wa katika utekelezaji wa Miradi .
“Ni viźuri wakati wa utekelezaji miradi katika jimbo la Ilemela mkahakikisha kunakuwa na matumizi sahihi ya fedha za maendeleo lakini pia uzalendo uwekwe mbele” alisema Dkt Mabula
Waziri huyo wa Ardhi na Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza alifanya ukaguzi wa miradi katika Kata ya Bugogwa, Shule ya Msingi Igombe ambapo serikali imetoa zaidi ya shilingi Milioni 69, 100,000 kupitia mradi wa Boost kufanikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa Shuleni hapo .
Moja ya mradi unaotekelezwa katika jimbo la Ilemela mkoa wa Mwanza
Lakini pia amefanya ukaguzi kata ya Kahama katika ujenzi wa Shule mpya ya Msingi inayojengwa kata ya Kahama ambapo serikali imetoa zaidi shilingi Milioni 540 ,300,000. kupitia mradi wa Boost pamoja na ukaguzi wa ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Buswelu – Busenga ambapo serikali pia imetoa zaidi tsh Milioni 540,300,000. kufanikisha ujenzi wa Shule hiyo .
Aidha, alifanya ukaguzi wa ujenzi wa Bweni la watoto wenye mahitaji maalum Shule ya Msingi Buswelu ambapo Serikali imetoa zaidi ya Milioni 100 kufanikisha ujenzi wa Bweni hilo na zahanati mpya iliyojengwa kata ya Ilemela mtaa wa Lumala ambapo zaidi ya Tsh Milioni 142 zimetumika kujenga zahanati hiyo ambapo pia Mhe Mbunge amechangia tofari zaidi 3500.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula akikagua miradi ya maendeleo katika jimbo la Ilemela mkoa wa Mwanza jana.
Akizungumza mara baada ya ukaguzi uliofanywa na Dkt Mabula katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Ilemela, Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela Hassan Milanga alimpongeza Mbunge wa jimbo hilo kwa uchapakazi wake ambapo alibainisha kuwa chama cha Mapinduzi wilayani humo kinatambua jitihada zake katika kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Ilemela
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza Hassan Masala alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuipatia Ilemela fedha nyingi za miradi na kueleza kuwa fedha hizo zinakwenda kutatua changamoto mbalimbali katika Wilaya ya Ilemela
Akihitimisha ziara hiyo, Waziri Mabula alitoa wito Kwa wananchi kuendelea kumuunga mkono Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa kazi kubwa ya maendeleo anayoifanya jimboni Ilemela
Aliwashukuru wananchi wa kata ya Ilemela Kwa kuendelea kuiamini serikali lakini pia Kwa ushirikiano wanaoutoa Kwa serikali .