Jeshi la Polisi kupitia chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kimeendelea kupata
elimu na maarifa kutoka kwa vyuo mbalimbali ndani na nje ya Nchi ambapo Taasisi ya
Maendeleo ya jamii Tengeru wametoa Elimu na mafunzo ya ukatili wa kijinsia katika
chuo cha taaluma ya Polisi Dar es salaam lengo likiwa ni kuwapa maarifa mapya
kukabiliana na matukio hayo.
Mwezesha wa mafunzo hayo Everlyne Rwela ambaye ni Mkuu wa idara ya Jinsia kutoka
Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru amesema kuwa wametoa mafunzo kwa askari
wa Jeshi la Polisi ambao ni wahusika wakubwa katika mapambano dhidi ya ukatili wa
wanawake na watoto ambapo amebainisha kuwa wamefundisha maswala ya ukatili wa
kijinsia.
Kwa upande wake Meneja wa kituo cha kitaifa cha utafiti na uhifadhi wa machapisho
yanayohusu wanawake kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Bi Rose Mtei
amesema kuwa waliona vyema kama taasisi watoe elimu ya ushirikishwaji jamii kwa
mifano ambapo amebainisha kuwa wataendele kuwekeza katika kufundisha wa
ushirikishwaji katika jamii ili kuwaongezea maarifa Jeshi hilo.
Nae Mkuu wa kitengo cha utafiti cha Jeshi la Polisi kilichopo chuo cha Taaluma ya Polisi
Dar es salaam amesema Kamishna msaidizi wa Polisi ACP Ralph Meela amebainisha
kuwa kuwa maafisa hao wanafunzi wanakwenda kutoa huduma bora Zaidi kutokana na
elimu na maarifa hayo mapya waliopata kutoka katika tasisi hiyo yanakwenda kujibu
changamoto za ukatili katika jamii ya watanzania.
Sambamba na hilo Mwanafunzi wa kozi ya mkaguzi msaidizi wa Polisi Artidius
Ryabugaba hamesema kuwa kutokana na elimu hiyo imewaongezea maarifa katika
kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Pia mkaguzi msadizi mwanafunzi Kangale Makweta amesema yuko tayari baada ya
mafunzo yake katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam Kwenda kuhudumia
wananchi baada ya kupaata mbini za kukabiliana na vitendo vya ukatili.