KITAIFA

DKT. YONAZI “TUTAENDELEA KUELIMISHA UMMA MASUALA YA MAAFA”

DKT. YONAZI “TUTAENDELEA KUELIMISHA UMMA MASUALA YA MAAFA”

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (mwenye suti) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa ofisi yake alipotembelea  banda la Idara ya Menejimenti ya Maafa katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge kupitia Idara ya menejimenti ya maaafa imesema itaendelea kutoa elimu kwa wananchi  juu ya namna ya kujikinga na majanga mbalimbali pindi yanapotokea ili kupunguza athari za majanga hayo.

Akizungumza hii leo Julai 6, 2023 wakati alipotembelea maonesho ya kimataifa ya 47 ya biashara maarufu kama sabasaba Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Dkt. Jim Yonazi amesema kuwa Serikali inaendelea Kushirikiana na wadau ili kuhakikisha kuwa uwezo wa nchi katika kukabiliana na majanga mbalimbali pindi yanapotokea unaboreshwa.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akiangalia moja ya kitambulisho cha waandishi wa habari (press card) wakati wa ziara yake banda la Idara ya habari maelezo, kulia ni Afisa habari Idara ya Habari maelezo Bi. Lilian Lundo.

Aliongezea kuwa, Serikali itaendelea kuratibu vyema masuala ya menejimenti ya maafa kwa kuzingatia mifumo ya kitehama ili kuwafikia wananchi kwa wakati kuendelea kuleta matokeo yanayokusudiwa.

“Serikali imewekeza katika mifumo mbalimbali ya kiteknolojia inayosaidia kutoa Viashiria vya awali vya majanga na pia kusaidia katika utoaji wa taarifa kwa haraka,”Alieleza Dkt. Yonazi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akiangalia moja ya kitabu wakati alipotembelea katika banda la Idara ya Menejimenti ya Maafa  lililochini ya ofisi yake katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) JIjini Dar es Salaama

Pia akieleza mikakati ya serikali kuratibu masuala ya maafa alisema imejipanga kuufikia umma wa Watanzania kuanzai ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya , Mkoa hadi Taifa na kwa kuzijengea uwezo kamati za maafa kwa ngazi zote na kuwa na jamii stahimilivu ya maafa nchini.

“Katika mwaka huu mpya wa fedha, tumejipanga kuendelea kujenga uwezo kwa wadau wetu ili kuhakikisha uwezo wetu wa kukabiliana na majanga aina mbalimbali unaboreshwa kwa kuzingatia athari zake kiuchumi, kijamii na nyingine nyingi,” Alisisitiza Dkt. Yonazi

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *