Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza katika Uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe wakati alipofanya ziara katika Mkoa huo ili kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI.
Serikali kupitia tume ya kudhibiti ukimwi TACAIDS imeongeza bajeti ya mapambano dhidi ya UKIMWI kutoka shilingi bilioni 14 katika mwaka wa fedha ulioisha hadi bilioni 25 katika mwaka mpya wa fedha 2023/2024 ili watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI waweze kupata dawa kwa uhakika na kuendeleza shughuli zao.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga, alipowatembelea watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI katika Halmashauri ya Mji wa Njombe ambapo alisema lengo la Serikali ni kuona WAVIU wanaendelea vyema na maisha yao huku wito ukitolewa kwa wanaume kujiunga kwenye vikundi pindi wanapobainika kuwa na maambukizi.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akitembelea mabanda ya wajasiriamali wanaofanya shughuli mbalimbali za kiuchumi kupitia Konga za watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI wakati wa ziara yake mkoani Njombe.
Pia alipongeza hatua ya uanzishwaji wa Konga katika kila Kata akisema hatua hiyo huwaleta pamoja kw akushirikiana katika shughuli za uzalishaji na kujiona ni sehemu ya nguvu kazi ya Taifa.
“Niupongeze Mkoa wa Njombe mmepiga hatua kubwa sana katika mapambano dhidi ya UKIMWI,kuanzishwa kwa Konga hizi katika kila Kata inaleta faraja kwa WAVIU kwani wanapata fursa ya kujadili mambo yao na kufanyiwa kazi ,”Alisema Mhe. Ummy.
Vilevile Mhe. Ummy alibainisha kwamba Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan imejizatiti kuhakikisha wananchi wake wanaimarika kiuchumi hivyo akawahimiza WAVIU kujitokeza kwa wingi kuchukua mikopo ili kuboresha shughuli zao.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akikagua zao la Parachichi linalolimwa na kikundi cha watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI cha Jikubali Uishi kwa Kujilinda (JIUKU) alipotembelea shamba hilo kujionea shughuli zao katika mtaa wa Wikichi, Kata ya Ramadhani Halmashauri ya Mji wa Njombe mkoani Njombe.
Katika hatua nyingine aliwahimiza wanaume kujitokeza kwa wingi kupima afya zao na kujitambua mapema hali zao na kuanza mara moja matumizi ya dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI
“Kwa mujibu wa takwimu inaonyesha watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI kwa Mkoa wa Njombe ni zaidi ya 63,000 huku wanaume takribani 31,372 kwa Mkoa mzima wamepima afya zao nitumie nafasi hii kupongeza konga zetu na wadau wa maendeleo wakiwemo NACOPHA pamoja na hamasa kubwa iliyotolewa na Mhe. Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”Alibainisha.
Aidha aliwasisitiza kutosita kujitokeza kuchukua mkopo wa asilimia 10 ambao hutolewa na Serikali kupitia Halmashauri pindi mfumo huo wa mikopo utakaporejeshwa tena.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akitembelea mabanda ya wajasiriamali wanaofanya shughuli mbalimbali za kiuchumi kupitia Konga za watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI wakati wa ziara yake mkoani Njombe.
Naye Mratibu wa UKIMWI Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwa. Daniel Mwasongwe alisema Halmashauri hiyo imefanikiwa kuwafikia wateja wapya 12,717 katika huduma ya upimaji kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi mwaka huu na kuwaunganisha na Huduma ya Dawa kwa waliokutwa na VVU.
Kwa upande wake Katibu wa Konga Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwa. John Msofu na Katibu wa Kikundi cha watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI Kata ya Ramadhani (JIUKU),Bwa. Rajab Safari kwa niaba ya WAVIU wamesema wamekuwa wakiendelea na shughuli mbalimbali za ujasiriamali ikiwemo kilimo cha Parachichi, Mbogamboga na Ufugaji jambo linalowasaidia kupunguza makali ya maisha.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akiwa katika picha ya pamoja na watendaji kutoka Ofisi hiyo, wadau kutoka NACOPHA , TACAIDS na washiriki mbalimbali wakati alipotembelea la shamba Parachichi linalolimwa na kikundi cha watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI cha Jikubali Uishi kwa Kujilinda (JIUKU) katika mtaa wa Wikichi, Kata ya Ramadhani Halmashauri ya Mji wa Njombe mkoani Njombe.
Hata hivyo Halmashauri ya Mji wa Njombe iliomba kutengenezwa kwa mfumo wa Alama za vidole kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi ili kurahisisha changamoto ya kupotea kwa watu wanaotumia dawa.
1 Comment
ラブドール えろcom has been the ultimate in realism and quality.The website provides an extensive range of customization options,