KITAIFA

WAZIRI DKT. CHANA AZURU BANDA LA WIZARA ASHUHUDIA VIPAJI VYA SANAA

WAZIRI DKT. CHANA AZURU BANDA LA WIZARA ASHUHUDIA VIPAJI VYA SANAA

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana Julai 10, 2023 ametembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ambapo ameshuhudia Taasisi za wizara hiyo zikitoa huduma kwa wananchi.

Akiwa katika Banda hilo, ameshuhudia michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa Draft, Netiboli pamoja na kazi zinazofanywa na Wadau wa Wizara hiyo wakiwemo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Sanaa za Ufundi na uchoraji.

Aidha, alishuhudia Sanaa ya jukwani kutoka kwa waimbaji Chipukizi ambao wamepatikana kupitia shindano lilioandaliwa Wizara kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) katika maonesho hayo pamoja na burudani ya Msanii wa Taarabu Isha Mashauzi.

Aidha, Mhe. Chana alipata nafasi ya kutembelea mabanda mengine ikiwemo Banda la Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Tigo, Vodacom pamoja Pamoja na Azam.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *