KITAIFA

PROF. MBARAWA: TUKIWEKEZA VIZURI ASILIMIA 67 YA MAPATO YA SERIKALI YATATOKA BANDARI YA DAR ES SALAAM

PROF. MBARAWA: TUKIWEKEZA VIZURI ASILIMIA 67 YA MAPATO YA SERIKALI YATATOKA BANDARI YA DAR ES SALAAM

Bandari ya Dar es Salaam imetajwa kuwa ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi na kwamba asilimia 37 ya bajeti ya Serikali inatoka Bandari ya Dar es Salaam, endapo itapata mwekezaji mzuri au mahili takribani asilimia 67 ya mapato ya Serikali yatatoka bandari hapo.

Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari katika ukumbi wa Hyatt Regency, Dar es Salaam leo Juni 14, 2023, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa Serikali inajenga miradi mikubwa na haitaendelea kila siku kupeleka bakuli na kuanza kuombaomba wakati kama nchi kuna rasilimali ambayo ikitumia vizuri itaweza kubadilisha uchumi wa Watanzania kwa asilimia kubwa.

“Tuko hapa kwa ajili ya kujenga na kwa maslahi ya Watanzania, ndio maana tumewaita hapa, kazi kubwa muende mkawaelimishe Watanzania, sio kila mtu anapata fursa ya kwenda kwenye ‘social media’, wengine hawapati.
Nyinyi ni watu muhumi sana katika nchi yetu, tumetoa elimu na tutaendelea kutoa elimu, amesema.

Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania (TPA) ilianzishwa kupitia sheria namba 17 ya mwaka 2004.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *