KITAIFA

RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA JECHA

RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA JECHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametuma
salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kifo cha
aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mhe. Jecha Salim
Jecha.
Kifo cha marehemu Jecha kimetokea tarehe 18 Julai, 2023 katika hospitali ya Lugalo
jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Rais Samia amepokea taarifa za kifo cha marehemu Jecha kwa majonzi na
masikitiko makubwa.
Vile vile, Rais Samia ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya aliyekuwa Rais
wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa kufuatia kifo cha Bernard
William Mkapa (Mwenye Mkuti) ambae alikuwa kaka yake.
Rais Samia amewaomba wanafamilia wote wawe na moyo wa uvumilivu katika
kipindi hiki kigumu cha majonzi na amewaombea marehemu wote wapumzike
mahali pema peponi, Amina.

Marehemu Jecha Salim Jecha

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *