KITAIFA

WIZARA YA HABARI, MAWASILIANO NA TEHAMA YAJIPANGA KUHAKIKISHA MAWASILIANO YANAKUWA NA TIJA KWA WATANZANIA

WIZARA YA HABARI, MAWASILIANO NA TEHAMA YAJIPANGA KUHAKIKISHA MAWASILIANO YANAKUWA NA TIJA KWA WATANZANIA

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imedhamiria imejipanga
kimkakati katika mwaka wa Fedha wa 2023/2024 kuleta mabadiliko makubwa ya
huduma za Habari, Mawasiliano na TEHAMA nchini zenye tija kwa watumiaji wote
nchini.
Hayo yamesemwa Jijini Arusha na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye, wakati wa akifunga Kikao Kazi cha Viongozi
wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Wizara yake. Mheshimiwa Nape alisema kuwa
katika mwaka wa fedha wa 2023/2024 Wizara itatekeleza mambo makubwa matano
ambayo yataboresha huduma za mawasiliano nchini na kuleta mabadiliko makubwa
katika utoaji wa huduma hizo nchini.


Akitaja jambo la kwanza alisema, “Nimezindua Kamati ya Ushauri ya Masuala ya
Kiseramajuzi. Kamati hiyo inasimamiwa na mimi mwenyewe na wajumbe wa Kamati
hii ni Wenyeviti wa Bodi zote za Taasisi zilizo chini ya Wizara. Lakini ipo Kamati
Tendaji ambayo itaongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara na hii wajumbe wake ni
Wakuu wote wa Taasisi zilizo chini ya Wizara. Hali kadhalika kutakuwa na Kamati ya
Wataalamu ambayo wajumbe wake ni Wakurugenzi wa Wizara na wale wa Taasisi
zilizo chini ya Wizara watakaowajibika kuishauri Kamati Tendaji. Kamati hii
itaongozwa na Naibu Katibu Mkuu. Kamati hizi zinakwenda kufanya kazi kubwa ya
kuleta mabadiliko makubwa kwenye Sekta” alisema Mhe. Nape.


Jambo la pili alisema ni Wizara kukamilisha Mkakati Mawasiliano wa Taifa kwa
Umma. “Kuna ombwe kubwa la uratibu wa shughuli za mawasiliano Serikalini.
Serikali imeona tatizo hilo na jinsi masuala ya Mawasiliano yanavyofanyika hasa
wakati wa dharura. Tunaenda kukamilisha Mkakati huu na kuanza kuutekeleza katika
mwaka huu wa Fedha wa 2023/2024” alisema Mhe. Nape.
Akizungumzia jambo la tatu, alisema kuwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari itatekeleza kwa ufanisi Mkakati wa Uchumi wa Kidijitali katika
mwaka huu wa fedha. “Tayari tumeandaa Mkakati wa Utekelezaji wa Mfumo wa
Uchumi wa kidijitali nchini. Tanzania inaenda kuwa ya mfano katika upatikanaji wa
huduma kwa njia za kidijitali na kuimarisha uchumi wetu” alisema Mhe. Nape.
Mheshimiwa Nape alisema jambo la nne ni kuhakikisha Wizara na Taasisi zake
zinatekeleza Dira ya Wizara kuhusu Huduma za Mawasiliano. Dira hiyo ni pamoja na
kwanza, kuhakikisha huduma za mawasiliano zinafika kwenye kila kona ya nchi hii.
Pili, pamoja na kupatikana kwa huduma hizo, amesema lazima huduma hizo ziwe na ubora wa hali ya juu, tatu, ni muhimu pia ziwe salama kwa wananchi wote na
waweze kuzitumia bila hofu. Tano, huduma za mawasiliano ziwe za gaharama nafuu
na ambazo wananchi wataweza kuzimudu. “na tano, nia yetu ni kuhakikisha huduma
zinakuwa na matokeo makubwa kwa watumiaji. Hii ikiwa ni pamoja na kubadilisha
maisha yao kwa ujumla kama vile kupata huduma mbalimbali za habari, mawasiliano
na teknolojia ya habari, kufanya malipo kwa kutumia TEHAMA na kadhalika”
alifafanua Mhe. Nape.


Hali kadhalika Mheshimiwa Nape alisema jambo la nne kubwa ni kuhakikisha kuwa
kila mwananchi anapata huduma zote zinazotolewa na Serikali na Taasisi zake kwa
kutumia namba maalumu ya utambulisho (Jamii Namba) atakayopewa kila
mwananchi. “Kila mtanzania awe na namba ya utambulisho ambayo itakuwa na
taarifa zake zote tangu anazaliwa hadi anaondoka duniani. Wizara na Taasisi zake
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tunakwenda kuhakikisha kuwa Jamii Namba
inaanza kutumika” alisema Mhe. Nape.
Suala la tano alisema ni kuimarisha huduma za Baraza la Ushauri la Watumia
Huduma za Mawasiliano. Alisema Baraza hili ni muhimu sana kwa watumiaji wa
huduma za mawasiliano nchini. Alibainisha kuwa kuna laini za simu takribani milioni
61 ambazo zinatumiwa na wananchi kupata huduma mbalimbali na ni muhimu
kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma za mawasiliano. “Ninawaomba wananchi
watoe ushirikiano kwa Baraza hili ili waweze kupata haki zao na kutetewa na Baraza
hili ambalo liko kwa ajili yao” alihitimisha Mhe. Nape Nnauye.
Akizungumza katika hafla ya kufunga Kikao Kazi hicho, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Bwana Mohammed Khamis Abdulla amezielekeza Taasisi zote chini ya Wizara ziwe na
utaratibu wa kufanya Vikao Kazi (Retreat) kila mwaka mara baada ya kikao cha
Viongozi. “Vikao Kazi hivyo viwe ni vya kujipanga jinsi ya kuweka mikakati ya
kutekeleza maazimio ya Kikao kazi cha viongozi na pia kujipanga jinsi ya kukabiliana
na changamoto za utekelezaji na maboresho ya utendaji kazi wa Taasisi na
kuanzimia kwa pamoja utekelezaji wa malengo ya mwaka wa fedha unaofuata”
alisema Bwana Mohammed Abdulla.
Kuanzia tarehe 19 hadi 22 Julai 2023, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Taasisi zake
(Shirikala Utangazaji Tanzania (TBC), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),
Baraza la Ushauri la Watumiaji huduma za Mawasiliano (TRCA-CCC), Shirika la
Mawasiliano Tanzania (TTCL), Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Tume ya
TEHAMA (ICTC), Shirika la Posta Tanzania (TPC), Shirika la Magazeti ya Serikali
(TSN) na Tume ya Kulinda Taarifa Binafsi. Viongozi Wakuu wa Wizara, Wenyeviti wa
Bodi, Wakuu wa Taasisi na Menejimenti zao walihudhuria Kikao kazi hicho.

About Author

Bongo News

28 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *