KITAIFA

SERIKALI KUTOA MILIONI 500 KWA AJILI YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA PERAMIHO – NDEJEMBI

SERIKALI KUTOA MILIONI 500 KWA AJILI YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA PERAMIHO – NDEJEMBI

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na wananchi wa Peramiho (hawapo pichani), mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango kumpatia fursa ya kuzungumza na wanachi wa eneo hilo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi
amesema, Mhe. Angellah Kairuki ameahidi kuwa Serikali itatoa milioni 500
kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Peramiho ikiwa ni utekelezaji wa
maelekezo ya Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango aliyoyatoa
mara baada ya Mbunge wa Peramiho Mhe. Jenista Mhagama kuwasilisha
ombi la kujengewa kituo cha afya.

Wananchi wa Peramiho wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango kumpatia fursa ya kuzungumza nao.


Mhe. Ndejembi ametoa ahadi hiyo kwa wananchi wa Peramiho kwa niaba
ya Waziri wa TAMISEMI Mhe. Angellah Kairuki, mara baada ya Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor
Mpango kumpatia fursa ya kuzungumza na wananchi hao.
Mhe. Ndejembi amesema kwa heshima na maelekezo ya Makamu wa
Rais, fedha hiyo itatolewa mapema iwezekanavyo ili kuwezesha ujenzi wa
kituo cha afya ambacho kitaboresha utoaji wa huduma za afya kwa jamii.
“Ujenzi wa kituo hicho cha afya unatokana na jitihada za Serikali ya Awamu
ya Sita ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge wa
Peramiho Mhe. Jenista Mhagama ambaye amekuwa mstari wa mbele
katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wake,” Mhe. Ndejembi
amesisitiza.
Ameongeza kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan hivi karibuni ataleta gari mbili za kubebea wagonjwa
katika Halmashuri ya Wilaya ya Songea, ikiwa ni sehemu ya muendelezo
wa maboresho ya utoaji wa huduma za afya katika Hamashauri hiyo.
Aidha, Mhe. Ndejembi amesema kuwa mafanikio ya Mhe. Rais Dkt. Samia
Suluhu Hassan Wilayani Songea na katika maeneo mengine yanajianisha
wazi kupitia kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya
elimu ya awali, msingi na sekondari.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *