KITAIFA

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAWAKARIBISHA WADAU, WANANCHI MAONESHO YA NANENANE 2023 MBEYA

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAWAKARIBISHA WADAU, WANANCHI MAONESHO YA NANENANE 2023 MBEYA

Watumishi wa Ofisi ya Makamu wakionesha nakala ya machapisho mbalimbali
yanayozalishwa na ofisi hiyo kwa ajili ya kutoa huduma kwa wateja
mbalimbali wanaotembelea Banda la Ofisi hiyo katika Maonesho ya Sikukuu ya
Wakulima Duniani (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya John
Mwakangale Jijini Mbeya leo Jumatano (Agosti 2, 2023)

Ofisi ya Makamu wa Rais imeungana na Wizara, Idara, Wakala na Taasisi za Umma na
Binafsi katika kushiriki Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Duniani (Nanenane) kitaifa yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Maadhimisho hayo yaliyozinduliwa jana Agosti Mosi, 2023 na Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Mpango yanatarajia kufikia kilele chake tarehe 8, 2023 ambapo Mgeni rasmi
anatarajia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan.
Katika maadhimisho hayo, Ofisi ya Makamu wa Rais inaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu ya ofisi hiyo ikiwemo elimu masuala ya Muungano na Hifadhi ya Mazingira kupitia Maafisa wa Idara hizo ambao wanatoa ufafanuzi na kujibu maswali mbalimbali ya wateja wanaotembelea banda hilo.

Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa
Rais, Bw. Abdallah Lungo akitoa ufafanuzi wa majukumu ya Idara hiyo kwa
wateja waliotembelea Banda la Ofisi hiyo katika Maonesho ya Sikukuu ya
Wakulima Duniani (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya John
Mwakangale Jijini Mbeya leo Jumatano (Agosti 2, 2023


Aidha, katika kuhakikisha elimu ya masuala ya Muungano na Mazingira inawafikia
walengwa, Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia maonesho hayo imeandaa machapisho
mbalimbali ikiwemo vipeperushi, magazeti ya zamani yanayohusu historia ya waasisi wa taifa na masuala mengine ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Elimu ya Muungano itakayotolewa kwa wananchi kwa njia ya maswali na majibu na
machapisho mbalimbali ikiwemo ikiwa ni pamoja Kitabu cha “Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Chimbuko, Misingi na Maendeleo”, Jarida la Ofisi ya Makamu wa Rais; na Magazeti ya zamani yenye habari kuhusu Muungano.
Kuhusu Mazingira, kupitia maonesho hayo Ofisi inaendelea kutoa elimu kwa wateja na
wadau kupitia machapisho mbalimbali ikiwemo Mkakati wa Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 na Mpango Kabambe wa Mazingira (2022-2032) unaoanisha hatua na mipango iliyoanishwa na Serikali katika usimamizi bora wa mazingira.

Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa tayari kutoka huduma kwa
wateja wanaotembelea Banda la Ofisi hiyo katika Maonesho ya Sikukuu ya
Wakulima Duniani (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya John
Mwakangale Jijini Mbeya leo Jumatano (Agosti 2, 2023)


Mpango wa Elimu kwa Umma kuhusu Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, Mabadiliko ya Tabianchi na fursa ya Biashara ya Kaboni ni eneo lingine litakalopewa kipaumbele kupitia maonesho ambapo kelimu kuhusu umuhimu wa uhifadhi na usimamizi wa mazingira itaendelea kutolewa kwa wadau na wananchi kupitia njia mbalimbali zikiwemo vyombo vya habari.
Maadhimisho ya Sikukuu ya Nanenane ambayo pia yanaendelea katika mbalimbali nchini yanachagizwa na kaulimbiu isemayo ‘Vijana na Wanawake ni msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula.’

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *