KITAIFA

WAZIRI JAFO ATETA NA WATUMISHI WA OFISI YAKE

WAZIRI JAFO ATETA NA WATUMISHI WA OFISI YAKE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa Ofisi yake wakati akifungua
kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma leo Agosti 3, 2023.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo amesema ushirikiano baina ya viongozi na watumishi wa Ofisi
ya Makamu wa Rais umechangia katika kudumisha Muungano na kuimarisha
usimamizi endelevu wa mazingira.
Dkt. Jafo ametoa kauli hiyo wakati akifungua Kikao kazi cha Watumishi wa
Ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dodoma leo Agosti 3, 2023.
Kutokana na hatua hiyo, Dkt. Jafo ameshukuru na kuwapongeza viongozi na
watumishi kwa ujumla kusukuma mbele ajenda ya mazingira kupitia usimamizi
wa kanuni na miongozi mbalimbali ya mazingira.
“Ndugu zangu watumishi nitoe pongezi za dhati kwenu kwani mmetumia
vyema utaalamu wenu katika kusimamia vizuri hifadhi ya mazingira kupitia
kampeni zetu mbalimbali za mazingira,“ amesisitiza.

Menejimenti na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa katika kikao
kazi cha watumishi wa Ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dodoma leo Agosti 3,
2023.


Pia, Waziri Jafo amewahimzia wasimamizi wa miradi inayotekelezwa na Ofisi
hiyo kuendelea kuisimamia vyema ili iendelee kueleta tija kwa wananchi katika
maeneo yenye changamoto za mazingira.
Amewahimiza watumishi hao kuishi kwa kupendana na kutimiza wajibu wao
kwa kufanya kazi kwa ufanisi na kwa kujituma ili kuacha alama nzuri.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga
amewahimiza watumishi wa ofisi hiyo kuwa wabunifu ili kupata matokeo
makubwa katika utekelezaji wa majukumu.
Pamoja na kuwapongeza watumishi hao, pia amewataka waendelee kufanya
kazi kwa juhudi na maarifa kwani kwa kufanya hivyo kutachangia katika
kusukuma mbele maendeleo.
Pia, ametoa rai kwa watumishi kupitia ubunifu na taalama zao watumie fursa
ya teknolojia inayopatikana ili kuboresha mazingra ya kazi na hivyo kufanya
utendaji wa kazi kuwa wenye tija.
“Kama mnavyojua sasa hivi tumeshaanza mwaka mpya wa fedha na hivyo
nina matarajio makubwa sana kutoka kwenu watumishi kuona mnafanya kazi
kwa bidii na hivyo Ofisi inapata matokeo mazuri,” amesisitiza Katibu Mkuu.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *