KITAIFA

WAZIRI JAFO: SERIKALI ITAENDELEA KUHAMASISHA UPANDAJI MIKOKO

WAZIRI JAFO: SERIKALI ITAENDELEA KUHAMASISHA UPANDAJI MIKOKO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge yatokanayo na Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Nane na wa Tisa wa Bunge iliyowasilishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma leo Agosti 09, 2023.

Serikali imesema itaendelea kuhamasisha upandaji wa mikoko katika maeneo
ya pwani kwa ajili ya biashara ya kaboni na kusaidia kukabiliana na athari za
mabadiliko ya tabianchi.
Amesema hayo wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria
Ndogo kuhusu Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge yatokanayo na Uchambuzi
wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Nane na wa Tisa wa
Bunge iliyowasilishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma leo Agosti 09,
2023.
Dkt. Jafo amesema kuwa ni kweli maeneo ya pwani yanapata changamoto ya
kuliwa na maji ya bahari kutokana na kina kuongezeka hivyo Serikali
inaendelea na jitihada za kukabiliana na changamoto hiyo kwa kujenga kuta
na matuta kwa ajili ya kupunguza kasi ya mawimbi ya bahari.
Amesema katika Biashara ya Kaboni Serikali inawakaribisha wawekezaji
kutumia fursa hiyo kwa kupanda mikoko katika maeneo hayo ya pwani yenye
changamoto hizo za kimazingira.
Amesema kuwa katika baadhi ya maeneo ya pwani mikoko inachukuliwa na
maji hivyo inasababisha kingo za bahari kumomonyoka hivyo maji huingia nchi
kavu na kusababisha mafuruko.
Aidha, Waziri Jafo amewahimiza wakulima kuendelea kulima zao la korosho na
kusema kuwa mbali ya kuwapatia faida wakati wa uvunaji pia watafaidika na
biashara ya kaboni hivyo kuunga mkono juhudi za kupunguza hewa ya ukaa.
“Tutaendelea kutoa elimu kwa halmashauri nchini wapate utaratibu mzuri wa
kuhusu kushiriki katika Biashara ya Kaboni kwani tayari tunashuhudia kule
wilayani Tanganika wamenufaika,” amefafanua Dkt. Jafo.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *