Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameridhia
uamuzi wa Serikali ya Indonesia wa kufufua shughuli za Kituo cha Mafunzo ya
Kilimo kwa Wakulima Vijijini (FARTC) kilichopo Mkindo mkoani Morogoro.
Rais Samia amesema hayo leo akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia
Joko Widodo aliyepo nchini kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili wakati
wakizungumza na vyombo vya habari.
Aidha, Rais Samia amesema kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 1996 na Serikali ya
Indonesia kimechangia kwa kiasi kikubwa kuelimisha wakulima na kutoa mafunzo
kwa wataalam wa kilimo.
Rais Samia pia amesema Tanzania na Indonesia zimekubaliana kukuza biashara na
uwekezaji kwa kuzileta pamoja sekta za umma na binafsi ili kuimarisha ushirikiano
katika viwanda, kilimo, nishati, madini, mafuta na gesi, uvuvi na utalii.
Vile vile, Rais Samia amesema majadiliano yao yamebainisha nia ya Tanzania kupata
uzoefu wa uzalishaji mafuta kutoka kwa Indonesia ambaye ni mzalishaji mkubwa
zaidi wa mafuta ya mawese duniani.
Hali kadhalika, Rais Samia amesema Serikali ya Tanzania imejidhatiti kuhakikisha
inaongeza uzalishaji wa mafuta ya kula ili iache kabisa kutumia fedha zake za kigeni
kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi.
Nchi hizo mbili zimetiliana saini hati 7 za Makubaliano (MoUs) ikiwemo sekta za
ulinzi, nishati, kilimo, mifugo, uvuvi na uchumi wa buluu, madini, na pia misamaha
ya viza kwa wamiliki wa hati za kusafiria za kidiplomasia na za huduma.
a huduma.
1 Comment
giving access to religious texts,ラブドールliterature,