BIASHARA KITAIFA

BENKI YA MADINI MBIONI KUANZISHWA, STAMICO YAANZISHA MCHAKATO, WACHIMBAJI KUKOPESHEKA

BENKI YA MADINI MBIONI KUANZISHWA, STAMICO YAANZISHA MCHAKATO, WACHIMBAJI KUKOPESHEKA

Shirika la Madini la Taifa(Stamico) limeanza mchakato wa kuanzisha Benki ya Wachimbaji Madini Tanzania lengo likiwa ni  kutafuta njia mbadala inayoweza kutatua kabisa vikwazo vya kimitaji kwa wachimbaji wadogo nchini.

Akizungumza leo Agosti 28,2023 wakati wa mkutano na wahariri wa vyombo vya habari, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico Dkt Venance Mwasse amesema  wachimbaji wadogo wanakosa mikopo katika taasisi za kifedha kutokana na kukosekana kwa dhamana.

“Taarifa zinaonyesha kuwa sekta ya madini ina sifa zake zisizoend seeana na mahitaji ya taasisi za kifedha, wanaona ni vigumu kuweka mikopo kwenye shughuli za tafiti kwa hiyo Benki ya wachimbaji itasaidia kukabiliana na changamoto hiyo,”amesema Dk Mwasse.

Kwa mujibu wa utafiti wa Stamico, wachimbaji wadogo wanakabiliwa na changamoto ya elimu ya uchimbaji, ukosefu wa taarifa, na teknolojia duni

Mwasse amesema baada ya utafiti huo Stamico iliandaa kalenda ya utoaji elimu huku ikiingia makubaliano na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) kwa ajili ya taarifa za mashapo.

“Tumeingia makubaliano (MOU) na GST ili kuwasaidia kupata taarifa za kijiolojia katika maeneo yao.

“Pia tumejipanga kufanya manunuzi ya mitambo mingine 10 ifikapo mwishoni mwaka wa Fedha 2023/24 Jumla ya mitambo itakuwa 15.”

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *