Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Leo September 20 amezindua Kiwanda Cha Kutengeneza Vioo Cha Sapphire Glass Ltd kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani.
Kiwanda hicho Cha kwanza Afrika mashariki na kati na Cha nne Afrika ambapo kina uwezo wa kuzalisha Tani 700 za Vioo kwa Siku.
Ujenzi wa Kiwanda umegharimu Zaidi ya Shilingi Bilioni 740 na kinatarajiwa kutoa Ajira kwa zaidi ya Vijana 1,600 na mpaka Sasa kimeajiri zaidi ya Vijana 700.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi huo, Rais Dkt. Samia amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira Bora na rafiki ya kuvutia wawekezaji nchini Ili kuchochea Maendeleo na kutatua changamoto ya Ajira.