KITAIFA

KAMPUNI YA CRC YABURUZWA MAHAKAMNI NA BENKI YA EQUITY,YADAIWA MABILIONI YA FEDHA ILIZOKOPA

KAMPUNI YA CRC YABURUZWA MAHAKAMNI NA BENKI YA EQUITY,YADAIWA MABILIONI YA FEDHA ILIZOKOPA

Kampuni ya usafirishaji ya Continental Reliable Clearing (T) LIMITED ( CRC) inahangaika kujinusuru na hatari ya kufungwa kwa amri ya mahakama baada kuwasilisha mahakamani maombi ya zuio dhidi ya Benki ya Equity ili hatua hiyo isitangazwe katika vyombo vya habari.

Kutokana na hali hiyo, Kampuni hiyo iko hatarini kufungwa kufuatia shauri la maombi lililofunguliwa na Benki ya Eguity, Equity Bank Tanzania Limited na Equity Bank Kenya Limited, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Masjala Kuu Dar es Salaam.

Katika hati ya mujibu wa hati ya maombi katika shauri hilo la maombi namba 517/2023, Benki hizo zinaiomba mahakama hiyo itoe amri ya kuifunga kampuni hiyo na kumteua msimamizi, kutokana na kushindwa kulipa madeni inayodaiwa na benki hiyo.

Hati ya maombi ya benki hizo zinazowakilishwa na kampuni ya uwakili ya Lior Attorneys, kampuni hiyo ya Continental ilichukua mikopo mbalimbali kwa ajili ya kuendeshea shughuli zake kutoka katika benki hiyo kwa nyakati tofautitofauti, tangu mwaka 2013 mpaka Aprili 2022.

Katika shauri hilo benki hizo zinaidai kampuni hiyo Dola za Marekani zaidi ya 10.5Milioni na fedha za Tanzania zaidi ya Sh780.6 milioni na kwamba kampuni hiyo imeshindwa au imepuuza kuzilipa licha ya kuiandikia taarifa ya kisheria kuitaka ilipe deni hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakili anayesimamia benki hizo ni Shalom Samuel Msakyi, alisema shauri hilo linalosikilizwa na Jaji Butamo Philip limepangwa kutajwa Oktoba 26, 2023 kwa ajili ya usikilizwaji wa pande zote mbili katika maombi madogo yaliyoletwa na wajibu maombi(CRC).

Hata hivyo kampuni ya Continental inayowakilishwa na wakili Frank Mwalongo nayo imefungua shauri la maombi madogo ikiiomba mahakama hiyo itoe maelekezo kwa benki hizo zisitoe matangazo magazetini ya kuifunga kampuni hiyo kama sheria inavyoelekeza, mpaka zitakapoelekezwa na Mahakama .

Wakili Msakyi amedai maombi madogo 532/2023 yalisikilizwa mwanzoni mwa wiki hii na Jaji Philip, ambaye baada ya kusikilizwa hoja za pande zote alitoa zuio la muda (benki hizo zisitoe matangazo hayo magazetini) mpaka Oktoba 26, 2023 maombi ya msingi yatakapotajwa.

About Author

Bongo News

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *