Uncategorized KITAIFA

TUNAENDELEA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA BARABARA NA MADARAJA: RAIS SAMIA

TUNAENDELEA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA BARABARA NA MADARAJA: RAIS SAMIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea na juhudi mbalimbali za kuimarisha miundombinu ya Barabara na Madaraja Nchini kwani ndio kilio cha wananchi kwa sasa.

Rais Samia amesema hayo wakati akizungumza na wananchi eneo la Itigi baada kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Makongolosi – Rungwa – Itigi – Mkiwa Kilomita 413 kwa kiwango cha lami; Sehemu ya Doroto – Noranga – Itigi – Mkiwa yenye urefu wa kilomita 56.9

Ameitaja baadhi ya Miradi ya barabara na madaraja iliyokamilika hivi karibuni katika Ukanda wa Kati ambayo ni Daraja la Sibiti (m 82); (Singida/Simiyu), Manyoni – Itigi – Chaya (km 85); (Singida), Tabora – Koga – Mpanda (km 360); (Tabora) na Tabora – Nyahua – Chaya (km 166.5); (Tabora)

Miradi mingine iliyokamilika ni Nzega – Tabora (km 116); (Tabora), Tabora Ndono – Urambo (km94); (Tabora), Urambo – Kaliua – Kazilambwa (km 86.9); (Tabora), Dodoma – Mayamaya – Mela (km 47); (Dodoma), Mwigumbi – Maswa (km 50.3) (Simiyu), Maswa – Bariadi (km 50) (Simiyu) na Bariadi – Lamadi (km 71.8) (Simiyu)

Naye Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kuwa, kuhusu Daraja la Sanza Daraja la Sanza na Maingilio yake yenye urefu wa kilomita 14.5 kwa kiwango cha lami, ambalo linaunganisha Mkoa wa Singida na Dodoma kupitia wilaya ya Manyoni eneo la Heka na Bahi eneo la Sanza, ambalo Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Dr. Pius Chaya amemuomba Mhe Rais na amekuwa akilipigania muda mrefu tayari kibali kimetolewa na usanifu na upembuzi yakinifu umefanyika na Mkataba wa Ujenzi umeshaandaliwa na unasubiri utiaji saini ili kazi iweze kuanza.

About Author

Bongo News

1 Comment

    After all, what a great site and informative posts, I will upload inbound link – bookmark this web site? Regards, Reader.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *